ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 18, 2011

Harusi Ya Maiga Na Jacqueline Kanisa La KKKT Azania Front Jijini Dar es Salaam

Bwana harusi, Maiga Dany Mapigano na Bibi Harusi Jacqueline Edmond Mjengwa. Leo jioni ilikuwa ni jioni ya kihistoria kwao. Ni katika kanisa la KKKT, Azania Front jijini Dar es Salaam, wamefunga pingu za maisha. Kanisani hapo palilindima shangwe, vigeregere na vifijo. Ni furaha ya Ndoa kati ya Maiga na Jackline.

Maiga na Jacqueline wakiwa wamepozi kwa utulivu kabisa wakati ibada takatifu ya Ndoa yao ikiwa inaendelea.
Maiga na Jacqueline (katikakati) wakiwa na wapambe wao. Ni jioni ya leo, akanisa la KKKT, Azania Front, jijini Dar es Salaam.

Maiga na Jacqueline wakivishana pingu za Maisha.
Maiga akisaini hati ya ndoa
Jacqueline akisaini hati ya ndoa
Wamekwisha ungana
Waumini wakiwa katika Ibada hiyo takatifu ya Ndoa.
Picha ya pamoja ya wanafamilia nje ya kanisa la KKKT Azania Front Cathedral, jijini Dar es Salaam, mara baada ya ibada ya Ndoa. Picha zote na Victor Makinda(MJENGWA BLOG)

No comments: