ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, July 17, 2011

HIVI LIKIZO INA UMUHIMU WOWOTE KWA MBEBA BOKSI

Kama sote tunavyofahamu, huu ndio msimu pekee wa jua katika nchi za Ulaya na Marekani ya kaskazini, pia ndio wakati muafaka wa kuchukua likizo ili kuchua migongo baada ya kubeba boksi kwa sana, na pia ni wakati mzuri wa kufurahi pamoja na familia (kwa wale wenye familia). Likizo sio lazima kwenda Bongo, kwani hata hapa kuna sehemu nyingi tu za kwenda na gharama yake ni ya kawaida kama ukijipanga.

Napenda kutumia fursa hii kutoa changamoto kwa wabeba boksi wenzangu tujitahidi basi tutafute muda wa kwenda likizo, kwani faida zake ni nyingi kiafya na hakuna hasara utakayoipata kwa kwenda likizo. Basi kwa wale ambao mmeshakwenda kwa mwaka huu tutumieni picha zenu na maelezo ya jinsi mlivyofaidi likizo zenu, pia tunaomba mchango wenu wa mawazo ni sehemu zipi mnadhani wabeba boksi wenzenu watafurahia kama wakitembelea....msisahau kutupatia makadirio ya gharama ya hizo sehemu.


By
 muwakilishi maalumu wa vijimambo.

5 comments:

Anonymous said...

kwanza wabeba box inabidi tutafute makaratasi halafu likizo,kwa muhamiaji ukiwa kwenye nchi ya mtu jambo la kwanza kufanya tafuta uhalali wa kuishi kwenye nchi hiyo halafu ndiyo tuonyeshane viatu mambo ya uhamiaji yanabadilika kila siku

wenu mbeba mabox.

Anonymous said...

Huo muda wa vacation, mngeutumia kwenda shule kujiendeleza.

Anonymous said...

Maharusi ya marekani yanavogarimu wabeba mabox unadhani wataenda likizo kweli.harusi hata Kama sio yako inagarimu tu this is how it goes.kutoa mchango,kununua nguo na wanavopenda kujishauwa wananunua nguo za grama kuna viatu kwa wadada nywele pia.ukijumlisha yote hayo si chini ya elfu dorali Kama ni couple,alafu harusi ziko every two mth everage kuna kwenda vakisheni kweli? Wabongo wanapenda maharusi sababu ya ubishoo na mashauzi kuliko vacations.eti mtu aende Miami beach hotel na kutembea tembea subutu.si bora avae suti au (wanake) gauni la nguvu ($300-500)essfront $500 original au $50 fake na kiatu pamoja na gucci fake akajishauwe harusini.mswahili na vacation wapi na wapi?

Anonymous said...

Kama hujabahatika kupata makaratasi, vacation haikufai. Na kama ulikuja ughaibuni kusoma halafu badala ya kusoma ikajiingiza kwenye kazi za kubeba mabox, basi napo vacation haikufai. Kinachokufaa kwa wakati huu na kutafuta namna ya kuachana na kazi za kubeba mabox kwa kuangalia namna ya kujitakasa kutoka kwenye janga la kutokuwa na makaratasi, kisha uingie kwenye shule na mambo yakinyoka unaachana na mabox. Kazi za mabox kwa watanzania zinatakiwa kuwa za muda na siyo za maisha yako milele.

Anonymous said...

Mimi ni mbeba bozi na nakwenda vacation kila mwaka hapa USA. Naishi DC; DE,VA,NJ, kuna bahari nzuri tu, huwa naendesha gari yangu mwenyewe Honda, unahaja ya kukodisha Range Rover. Hoteli ni kati ya $80-$150 per night. Chakula ni reasonable na mara nyingi hoteli nyingi zinatowa free breakfast. Chakuna cha mchana ni reasonable na kama unataka unaweza kula MCDonals. KFC, Wendys au unaweza kwenda kwenye good restaurant.

Ushauri wangu wa bure ni;
Usiende wakati wa Holidays
Kama una mtoto 1 mkapa wa 3, mnaweza wote mkakaa kwenye chumba kimoja.

Na wale wanaopondea kubeba BOKSI, kawaambia nani kuwa Kubeba Boksi si kazi? Tuacheni kashfa. Kwani Watanzania 45 millions wanaoishi Tanzania ni wangapi wamekwenda shule?