NENO LA VIJIMAMBO
Utawakuta Baba na Mama ni Watanzania wanaoishi UGHAIBUNI lakini watoto wao Kiswahili ZERO,hii kwangu mimi inasikitisha sana na sijui inatokana na nini hasa,watoto hata kuamkia shikamoo,ni ZERO.
Utakuta mataifa mengine kama vile Waspanishi wanaoishi nje na kwao,watoto wao wanaongea lugha ya Nchi hiyo pamoja na ya kwao vizuri kabisa,sasa kwa nini watoto wetu washindwe kufanya hivyo,nani alaumiwe,mzazi au mtoto?
Wazazi msisahau kuna usemi usemao
"MKATAA KWAO NI MTUMWA"
9 comments:
Mbona wewe hujui kuongea kitareme,
Ni kweli kaka. Halafu utamkuta mtu huyo huyo akizungumza na ndugu zake kwa njia ya simu toka bongo, basi anawasifia watoto wake kuwa wanajua kiingereza kweli.! Mimi napenda kusema kuwa watoto wafundishwe lugha zote kwani hivi sasa nchi hii inaajiri watu hasa wanaoweza kuzungumza lugha zaidi ya moja. Na kwa taarifa yenu tangu Januari hadi Juni mwaka huu Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeajiri zaidi ya watu 30 toka Afrika mashariki na kati hasa Native wenye uraia au kuzaliwa nchi hii toka nchi za TZ, Kenya, UG, Rwanda, Burundi, Sheli sheli na kati ya hao 12 wanatoka TZ. So, siyo jambo la kujivunia mtoto kuzungumza kimombo peke yake. Tujitahidi kuwafundisha na lugha yetu ya Taifa jamani. Tusione sifa mtoto kuzungumza kiingereza wakati hawezi kuwasiliana na Wajomba, Mababu na Mabibi na ndugu wengine kule nyumbani.
mimi sikubaliani na swala kwanini watoto wanaozaliwa huku na wazazi wakitanzania, kuwa hatutataki kuwafundisha kiswahili. kuna mambo mengi yanayo changia huku, kama wazazi wote wawili inabidi wakabebe mabox, mtoto kuanzia miezi labda mitatu anakaa muda mwingi kwa ma baby sitter/daycare, sasa huo muda wamtoto kujua kiswahili utatoka wapi. wenzetu waspanishi wengi wao wana extended family ambao ndio wanawasaidia kulea watoto kama wazazi wote wanafanya kazi.kwahiyo mtoto anakulia anasikia kispanish kuanzia mwanzo.Hamna wa kumlaumu mzazi au mtoto ni mazingira na maisha kwa ujumla. watoto wangu wanasikia kiswahili lakini hawezi kuongea na tunawapeleka tanzania atleast kila baad ya miaka miwili kuwaona wajomba, bibi na babu.
Babu we Kiswahili lugha ya umbeya itawasaidia wapi?
Mawazo ni mazuri ingwa kuna kidogo kuoneana. Labda ni kwa kuweka sawa hoja ili isitoke umakinifu. Ajira hizo unazozizungumzia hazitokani na uzungumzaji au ujuzi wa lugha ya kiswahili. Ingawa namba ya watu walioajiriwa kwa ajili ya lugha ya kiwahili, hapa marekani ni kubwa zaidi ya hiyo.
Kufananisha Waspanish na Waswahili katika kutupa lugha kwa ajili ya kiingereza ni kama kufananisha duriani na fenesi.
Asilimia kubwa ya waspanish waliokuja huku ni wale wasiosoma na hawajui hata kuomba maji kwa kiingereza. Wake zao wanakaa nyumbani na waume wanatoka kwenda kutafuta. Wanawake hawa hawawezi kuwasiliana na watoto wao kwa lugha ya kiingereza. Hivyo wanalazimika kutumia lugha ya kispanish kuweka sawa mawasiliano.
Waspanish ni wengi na wana community zao, ambazo zina kila kitu au wingi wa mahitaji yao, bila kutoka nje ya community zao.
Mfano huu utauona vizuri kwa Watanzania wanaoishi Uingereza.
Wewe unaishi na mkeo, nyote mnakwenda kazini. Mmetoka kwenu mnajua kiingereza cha kuombea maji. Hukutani na watanzania mpaka weekend au kwenye party. Kaka hapa utata lazima upatikane.
Ilimtoto wako ajue kiswahili,lazima ufanye kazi ya ziada sio kwa taratibu ya mazowea.
Kujua kiswahili sio kukubali kwenu, na kutojua sio kukataa kwenu. Mambo ni uzalendo kama sio mzalendo hata ujue kijapani kitupu utashiba tu maji ya meusi.
kwa kuengezea tuu... mimi ni mtanzania na mume wangu ni muarabu na tupo uingereza.... mimi naongea na mwanangu kiswahili na baba anaongea na mwanae kwa kiarabu na lugha zote mtoto anafahamu lkn hata siku moja hajajibu kwa lugha hizo yeye ni kiingereza tuu... na sote ni watu wa makaazini siku nzima anashinda kwa childminder ambae ni mzungu...hapo kwa kweli sometimes wazazi tunalaumiwa lkn iko nje ya uwezo wetu... unajitahidi na mtoto lkn kama hayuko tayari huwezi kumlazimisha vyema wa kwetu ni kwamba angalau anaelewa na ni kwanza 3yrs...kwahiyo kabla hatujalaumika angau kwanza mtu aulize kulikoni am sure kila mtu anagoodreason labda wachache ambao ni malimbukeni...
Kweli schedule ndiyo mambo yote hayo,ila ulimbukeni nao unanafasi yake eti jitu zima nilijisifa mie mwanangu chakula cha kitz chanini?auk kiswahili chanini wanajiona wamefika,mtuameingia hapa anamiaka 16 leo hii anakwambia amesahau lugha yake kweli hiyo au ndiyo nini vijimambo usishangae kuna wengine ukijulikana unapenda sana utz hata kwao hawakutaki
Waspanishi wanaongea lugha yao kwa kuwa pia idadi yao ni kubwa kulinganisha na mataifa mengine wageni wengine nchini Marekani.Hata shuleni pia wanapewa kipaumbele cha kuendeleaza lugha,Ndo maana wanashule. Mie ni MTz nyumbani tunaongea kiswahili na mtoto wetu pia anaelewa maneno ya kiswahili ila anachanganya na kiigereza. Lakini akiwa shuleni masaa 8 anaongea kiiengereza; akienda kwa mwangalizi wake pia ni kiingereza.
Kwahiyo basi mtoto akiongea kiingereza mwache kwani bado ni mdogo akikua atachagua lugha ya kuongea.
Nisawa wazazi kwa maoni yenu au mchango wenu, ila lugha yetu niyetu ni vizuri watoto wetu wajuwe hata cha kuombea maji hicho kiswahili!!!
Post a Comment