Juu na chini ni Mrisho Ngaza akiwa mazoezini leo na timu yake anayofanyia majaribio ya Seattle Sounders
Mrisho Ngasa baada ya mazoezi ya leo akisaliamiana na mashabiki wake Watanzania wanaoishi Seattle hawapo pichani.
Mrisho Ngasa akifanyiwa mahojiano na Dauda Shaffih
Kutoka kushoto ni Mudrick Maajaliwa,Mrisho Ngasa,Dauda Shaffih na Montero(picha kwa hisani ya Mudrick Maajaliwa,Seattle,WA)
Ibrahim Bakari, Nairobi
MSHAMBULIAJI wa Tanzania, Mrisho Ngassa ataanza katika kikosi cha kwanza cha timu Seattle Sounders itakapopambana na Manchester United kwenye Uwanja wenye nyasi bandia wa CenturyLink ikiwa ni mchezo wa kirafiki. Manchester iko Marekani ikijinoa kwa
mechi za kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu ya England baadaye mwezi ujao.Mwandishi wa Habari wa Seattle Sounders, Joshua Mayers aliiambia Mwananchi hapa Nairobi kuwa Ngassa ni kati ya wachezaji wanaotarajiwa kuwa katika kikosi cha kwanza katika mchezo wa (leo) utakaoanza saa 1:00 saa za Seattle, Marekani sawa na saa 8:00 usiku saa za Tanzania.
"Ninachoweza kukwambia ni kwamba, hakuna kilichobadilika, Ngassa atacheza mechi hiyo...kama mlivyoelezwa basi itakuwa hivyo, siwezi kukupangia kikosi kitakachocheza kwa kuwa kocha hajatangaza, lakini Ngassa yumo kikosini," alisema Mayers kutoka mji wa Seattle, Marekani.
Alisema kuwa Ngassa amekuwa gumzo katika viunga vya Seattle na kila mmoja anataka kumuona katika mchezo huo wa Manchester United ikiwa ni mechi ya kwanza kubwa mwaka huu.
Ngassa aliyekuwa akikipiga katika klabu ya Azam, alikwenda Marekani wiki iliyopita kwa ajili ya majaribio ya wiki mbili na endapo atafuzu, atakuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kujiunga na klabu hiyo ya Marekani iliyowahi kufanya ziara Tanzania mwaka 2008.
Juzi Jumatatu, Sounders FC iliyoshinda mechi 11 za ligi na kirafiki bila kupoteza hadi sasa, ilikuwa ikifanya mazoezi kwenye Viwanja vya Microsoft vya Redmond na yalikuwa mazoezi maalum kwa ajili ya kuwaonyesha mabosi na viongozi mbalimbali wa timu pamoja na familia zao kuja kuwaona wachezaji wao.
Timu ilikuwa katika mazoezi ya kawaida, iligawanywa katika makundi manne, wakifanya mazoezi ya wanne wanne na baadaye kutengeneza timu kwa mazoezi ya watano watano huku wachezaji wakifunga upande wowote wanaokaribia.
Jana Sounders ilifanya mazoezi kwenye uwanja wake wa Starfire tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya Manchester United utakaopigwa CenturyLink.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Sigi Schmid ambaye aliwashukuru wadhamini mbalimbali kuidhamini timu yake, aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao. "Wachezaji wanapoona umati wa mashabiki, wanapata nguvu zaidi, nadhani itakuwa vizuri wakija kwa wingi.
VANCOUVER, Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfani alishindwa kuisaidia timu ya Vancouver Whitecaps kuepuka kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Manchester City.
Khalfan aliingia kipindi cha pili wakati timu yake ikiongoza kwa bao moja lililofungwa na Camilo dakika ya 13 kwa shuti kali ambalo lilimgonga beki wa City, Stefan Savic na kujaa wavuni.
Mabingwa hao wa Kombe la FA waliamka na kupata bao la kusawazisha kupitia kwa John Guidetti dakika 68 kabla ya Shaun Wright-Phillips kupachika goli la ushindi kwa shuti la umbali wa mita 30 lililomshinda kipa wa Whitecaps,Jay Nolly na kutinga wavuni kwenye mchezo ambao ulishuhudiwa na mashabiki 24,074 kwenye Uwanja wa Empire Field.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment