
Ni wiki nyingine tena tunakutana kwa ajili ya kujifunza nguvu ya tunda jingine katika ustawi wa afya yetu. Leo tunaangalia faida za tango kiafya.
Kama ilivyokuwa kwa makala mbili zilizopita kuhusu kitunguu na nyanya, tango nalo ni tunda linalojulikana na kila mtu, sidhani kama kuna mtu hajawahi kulila, kama yupo namshauri aanze leo.
Kama ilivyokuwa kwa makala mbili zilizopita kuhusu kitunguu na nyanya, tango nalo ni tunda linalojulikana na kila mtu, sidhani kama kuna mtu hajawahi kulila, kama yupo namshauri aanze leo.
Tango lina virutubisho vingi na madini muhimu sana katika mwili wa binadamu. Kwa mujibu wa wataalamu wetu, miongoni mwa virutubisho na madini mengine yaliyomo, tango ni chanzo kizuri cha Kashiamu, Chuma, Phosforas, Potasiamu, Zinki, Kambalishe, Vitamini B complex, Vitamini C na Vitamin E.
FAIDA ZAKE MWILINI
Unaweza kusema kuwa kirutubisho cha ‘Potasiamu’ ndiyo chakula cha moyo, kwa sababu ‘potasiamu’ ndiyo inayouwezesha moyo kupiga mapigo yake ya kawaida na kuustawisha. Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha ‘potasiamu’ kama tango, ni muhumi sana kwa mtu mwenye matatizo ya moyo, presha ya kupanda na matatizo ya mapigo ya moyo.
Aidha, tango linaaminika kupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (cholesterol), huimarisha misuli ya mwili na bila kusahau husaidia usagaji wa chakula tumboni hivyo kuondoa tatizo la ukosefu wa choo.
Virutubisho vilivyomo kwenye tango pia, hutoa afueni kwa mtu mwenye matatizo ya ini, kongosho, figo na matatizo katika kibofu cha mkojo. Wataalamu wetu wanatueleza pia kuwa tango lina kirutubisho kinachojulikana kama ‘erepsin’ ambacho husaidia uzalishaji wa ‘amino acids’ ambazo ni muhimu kwa uzalishaji wa protini mwilini.
Vile vile, tango lina kiwango kingi cha Vitamin C, hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo yatokanayo na ukosefu wa Vitamin C, kama vile kutokwa na damu kwenye fizi, upungufu wa damu kwa watoto wachanga na kuota meno na mifupa vibaya.
KINGA YA SARATANI
Pengine faida kubwa kuliko zote unazoweza kuzipata kwa kula tango au juisi yake mara kwa mara ni kinga dhidi ya saratani za aina mbalimbali. Jambo hili linatokana na ukweli kwamba tango lina kiwango kikubwa cha ‘alkaline’ (uchachu). Kwa kawaida ‘seli’ za saratani ‘haziwezi kuishi’ kwemye mazingira yenye uchachu, hivyo tango kinga dhidi ya saratani.
DAWA YA MAGONJWA YA NGOZI
Tangu enzi na enzi, tango limekuwa likitumika katika masuala ya urembo wa ngozi, watu wengi hutumia tango kwa njia mbalimbali kutunza ngozi zao na kupendezesha sura zao. Hata baadhi ya vipodozi visivyo na madhara, hutengenezwa kutokana na tango.
Ulaji wa tango na unywaji wa juisi yake mara kwa mara, huondoa matatizo mengi ya ngozi yaliyomo ndani na nje ya mwili. Utakapotumia juisi ya tango kwa muda wa wiki mbili hadi tatu mfululizo, utakuwa na ngozi nyororo na yenye afya kushinda hata mtu anayetumia vipodozi.
JINSI YA KUANDAA JUISI YA TANGO
Ni rahisi sana, chukua tango lako moja au zaidi, lioshe vizuri na limenye, kisha katakata vipande tayari kwa kusaga, ama kwa mashine (blender/juicer) au kwa kutwanga kwenye kinu maalum, changanya na maji masafi kiasi ili kupata juisi kiasi cha glasi moja.
Unaweza kuweka sukari kiasi kidogo sana (kisizidi kijiko kimoja kwa glasi) ili kupata ladha au weka asali kijiko kidogo kimoja. Utapata matokeo mazuri na ya haraka kama ukinywa juisi yako kila siku asubuhi kabla ya kula kitu chochote.
Ili kutibu matatizo ya ngozi uliyonayo au magonjwa mengine kama tulivyoyaeleza hapo juu, kunywa juisi hiyo kwa muda wa wiki mbili hadi 4 mfululizo na angalia matokeo yake. Kwa ukuwaji wa afya yako, weka mazoea ya kunywa japo mara mbili au tatu kwa wiki.
Vile vile, unaweza kujiwekea mazoea ya kula tango kwa njia mbalimbali kama vile kuchanganya na saladi, kachumbari au kutafuna lenyewe mara kwa mara, kwani faida zake mwilini ni nyingi.
No comments:
Post a Comment