
MBUNGE mteule kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mussa Khamis Silima, ambaye alipata ajali juzi katika aneo la Nzuguni, Dodoma, amefariki dunia leo. Pichani juu: Marehemu akiwa katika machela baada ya kushushwa kwenye gari juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, alikoletwa na ndege kutoka Dodoma pamoja na gari alilopata nalo ajali. Mke wa marehemu, Mwanaheri Fahari nae alifariki katika ajali hiyo na kuzikwa jana na dereva wao Chezani Sebunga alijeruhiwa.

1 comment:
Mungu amlaze mahali pema peponi. Inakuaje wapigapicha wanatangulia mbele kabla ya wauguzi na hata haonekeni kuwa na muhudumu wa maana zaidi ya watu wananyosha vidole etc. Hamna machine wala dawa wala vipimo? Naona kidaftari juu yake tu. Can we honestly say all efforts were done to save this person's life? I doubt kama kila jitahada ilifanywa kumsave maisha yake (jmo)
Post a Comment