Andrew Mitchel(MP)
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa Andrew Mitchell leo amezuru mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Hii ni ziara ya kwanza kwa kiongozi wa serikali ya Uingereza kwenda Mogadishu kwa zaidi ya miongo miwili.
Mapema mwaka huu alikuwa Hargeisa, mji mkuu wa Jamhuri ya Somaliland.
Uingereza imeongeza mara tatu zaidi ya misaada yake kwa Pembe ya Afrika. Hatua hiyo inaonyesha kufufuliwa upya kwa ushiriki wa Uingereza katika masuala ya Somalia.
Yusuf Garaad wa idhaa ya Kisomali ya BBC ametathmini uwezekano wa Uingereza kufufua ushiriki wake katika Umoja wa Afrika.
Alisema kuna wasomali takriban 250,000 nchini Uingereza. Wengi wao husafiri kati ya nchi hizi mbili na hasa wanafunzi ambao huenda Somalia wakati wa likizo zao za shule.
Tishio la vijana wa asili ya Kisomali kukumbwa na nadharia za msimamo mkali si jambo ambalo serikali yoyote ya Uingereza ingelivumilia.
Somalia ina mwambao wa kilometa elfu tatu ambao ndio mrefu kupita yote barani Afrika. Ni mwambao mojawapo ulio na harakati nyingi za usafiri wa meli za mafuta na nyingine za kubeba mizigo.
Njia hiyo ya bahari huziunganisha Afrika, Ulaya na mwambao wa Mashariki ya Amerika na Uchina , Japani na nchi nyingine za Asia.
Maharamia wa Kisomali wametawala katika njia hii muhimu ya baharini.
Wanashambulia meli na kudai fedha nyingi kama kikombozi na mamilioni ya dola yamekwishalipwa.
Baadhi ya watu wanahoji kwamba ni baadhi ya fedha hizo hizo zinachangia kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia.
Kuna wengine ambao hata wanadai kuwa maharamia wanashirikiana na kundi la Alshabab.
Al Shabab, ni kikundi cha siasa kali za kiislamu kinachofungamana na Al Qaeda.
Ina kinachoipiga vita serikali ya mpito ya Somalia na washirika wake. Kimedai kuhusuika na mashambulizi ya Kampala ambapo zaidi ya watu 70 waliuawa.
Serikali ya Uingereza inaelekea imejitolea kufuata sera ya kuangalia mambo kwa jumla kuhusu matatizo ya Somalia.
Serikali ya Uingereza inaelekea imejitolea kufuata sera ya kuangalia mambo kwa jumla kuhusu matatizo ya Somalia.
Imeongeza zaidi ya maradufu wanabalozi wake nchini Somalia katika kipindi cha miaka michache iliyopita.
Tishio la usalama pamoja na janga kubwa linalowakabili wananchi ndio sababu zinazoifanya Uingereza kuongeza mara tatu msaada wake kwa Somalia kufikia zaidi ya dola millioni 130 kila mwaka katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
No comments:
Post a Comment