Umoja wa Mataifa umeziomba pande zote katika vita vya Libya, kuzuwia vitendo vya kulipiza kisasi.
Taarifa hiyo imetolewa baada ya kuarifiwa kuwa wanajeshi wa Kanali Gaddafi wameuwa watu, na kwamba Waafrika waliokuwa wakipigana kwa niaba ya serikali piya wameshambuliwa.
Huku kukiwa na ripoti kuwa Waafrika waliokuwa katika jeshi la Kanali Gaddafi wanauwawa, wengi wao wamekuwa wakivuka mpaka na kuingia Mali na Niger.
Inaarifiwa magari 60 yameingia Niger kutoka Libya, lakini yalizuwiliwa mjini Agadez.
Watu hao wengi ni wapiganaji wa zamani wa kabila la Tuareg, ambao walipatana na serikali ya Niger mwaka 2009.
Inaarifiwa kuwa magari 10 nayo yameingia Mali.
Mapema mwaka huu, wakuu wa Mali waliiambia BBC, kwamba Wa-Tuareg wakilipwa dola elfu 10 kujiunga na serikali ya Libya, na kila siku ya mapigano wakipata dola 1000.
Duru za mataifa ya magharibi zinasema Waafrika kama elfu 10 waliajiriwa na Gaddafi.
Sasa ndege za Nato zinarusha vikaratasi na kutoa matangazo, kuwasihi Waafrika waasi na watapokelewa kufwatana na sheria.
No comments:
Post a Comment