Wafanyakazi wakijaza viloba vya michanga ili vigawiwe kwa wakaazi wa DC hii ilikua kabla ya Tufani ya IRENE haijamwaga radhi na hapa ilikua ni karibu na uwanja wa R.F.K. Aug 27,2011.Tufani ya IRENE imemwaga radhi ghuba ya mashariki ya North Calrolina baada ya kugusa ardhi leo asubuhi na ksababisha mafuriko na upepo mkali ulioangusha miti na kusababisha wakaazi wa huko kukosa umeme
Charlene Tyler akichukua viloba vya michanga wakati wa ugawaji wa viloba hivyo kwa wakaazi wa DC hii ilikua ni kabla tufani ya IRENE haijatua DC.
Kikundi cha mabaharia kikifanya mazoezi ya mbio katikati ya mitaa ya Kapitali hii ilikua ni wakati mvua zilipokua zikiendelea kunyesha Washington,DC
Watalii ndani ya Kapitali wakihangaika na mvua yenye upepo iliyokua ikiendelea kunyesha Kapitali hii ilikua ni rasha rasha za kuwasili kwa tufani ya IRENE Washington,DC.
Watalii wanaotembelea Kapitali wakihangaika na mvua yenye upepo wakati walipokua wakitembelea Kapitali kabla ya tufani ya IRENE haijaanza kumwaga radhi,DC
Kama unavyoona kwenye UKodak huu jinsi gani Watalii wanaotembelea Kapitali wanavyopata shida na mvua zinazoendelea kunyesha mjini hapa zinazo ambatana na tufani ya IRENE ambayo tumeambiwa kama huna kitu muhimu cha kufanya ni bora ukae ndani kwani mvua zinazoendelea kunyesha na upepo mkali unaoweza sababisha maafa.
No comments:
Post a Comment