ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 15, 2011

Chameleon alivyobadili dini kuwa Muislam

Mwanamuziki aliye juu Uganda, Joseph Mayenja ‘Jose Chameleon’ Ijumaa iliyopita alibadili dini kuwa Muislam, jina pia amebadilisha na sasa anaitwa Gaddafi.
Staa huyo ambaye Bongo anakubalika mbaya, alibadili dini kwenye Msikiti wa Kibuli, Kampala, Uganda.

Chameleon, alifika msikitini hapo akiwa na gari la kifahari, huku akiwa amesindikizwa na wasanii, Haruna Mubiru na Grace Sekamate ambao wanapiga mzigo Studio ya Eagles Production.

SABABU
Mkali huyo Dancehall-Reggae ameeleza kwa kifupi tu sababu ya kubadili dini kuwa ameona Uislam ndiyo dini ya kweli na kwamba aliona awahi kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Alisema kuwa amependa aitwe Gaddafi kwa sababu anavutiwa na Rais wa Libya, Muammar Gaddafi.

MKEWE VIPI?
Miaka minne iliyopita, Chameleon alifunga ndoa ya Kikatoliki na mkewe wa sasa, Atim Daniella kwenye Kanisa la Mbuya lakini haijaelezwa hatma ya ndoa yake hiyo.

Picha kwa hisani ya redpepper na global pulishers

No comments: