BILA shaka unapoingia dukani au supermarket kununua juisi ya box, huwa unaamini kuwa iliyoandikwa ‘100% Puer Juice’ huwa ni halisi na ndiyo bora. Kwa kukuongezea imani zaidi, watengenezaji wameweka na neno ‘No Sugar Added’ au ‘No preservatives’ (haikuongezwa sukari wala dawa)!
Kuanzia leo elewa kwamba hayo ni maneno ya kibiashara tu, ukweli hauko hivyo! Umewahi kujiuliza kwa nini maboksi yote ya juisi hiyo yawe na ladha moja tu. Sote tunajua kwamba, kama ni juisi ya machungwa kwa mfano, ukila machungwa matano, yote hayawezi kuwa na ladha moja!
Kuanzia leo elewa kwamba hayo ni maneno ya kibiashara tu, ukweli hauko hivyo! Umewahi kujiuliza kwa nini maboksi yote ya juisi hiyo yawe na ladha moja tu. Sote tunajua kwamba, kama ni juisi ya machungwa kwa mfano, ukila machungwa matano, yote hayawezi kuwa na ladha moja!
Lakini kwa juisi za maboksi imewezekana kuwa na ladha moja kwa sababu za kikemia zinazofanywa kiwandani wakati wa kuhifadhi juisi hiyo ambayo huweza kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika. Hivyo siyo kweli kwamba unachokunywa ni asilimia 100 ‘pure’.
NINI KINACHOTOKEA?
Ni kweli kwamba ‘100% pure juice’ hutokana na matunda halisi kama vile machungwa, mananasi, embe, n.k, lakini mchakato wake wa kukamua, kuhifadhi na hatimaye kumfikishia mlaji ndiyo wenye dosari za kiafya.
Kinachofanyika baada ya tunda kukamuliwa ni kuhifadhi juisi yake kwenye matanki maalumu makubwa ya viwandani. Ili juisi hiyo iweze kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika, wanalazimika kuondoa hewa yake asilia ya oksijeni (mchakato unajulikana kitaalamu kama ‘deaeration’), kitendo ambacho huifanya juisi hiyo kupoteza ladha yake ya asili.
NINI HUFANYIKA KUREJESHA LADHA YA MATUNDA?
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Food Renegade’ wa nchini Marekani unaojishughulisha na masuala ya lishe na kuhimiza ulaji wa vyakula asilia, makampuni yanayozalisha juisi hukodisha makampuni yenye ujuzi wa kutengeneza ladha mbalimbali za matunda na manukato.
Makampuni hayo husimamia utengenezaji wa maboksi ya kuhifadhia juisi ambayo huwekwa ladha na harufu ya matunda husika. Inaelezwa zaidi kuwa makampuni hayo ndiyo yanayotengeneza pia manukato (perfumes) maarufu duniani, kama vile Dior na Calvin Klein.
Lakini cha kushangaza, virutubisho vinavyotumika kutengenezea ladha hiyo bandia haviorodheshwi kwenye boksi na wenyewe wanajitetea kwa kusema kuwa ladha hiyo haiwezi kuorodheshwa kama sehemu ya ‘ingredients’ kwa sababu hutengenezwa kutokana na tunda lenyewe, ingawa wataalamu wengine wanadai utengenezaji wake huhusisha kemikali zingine ambazo siyo za asili.
Mtaalamu mwingine kutoka Taasisi ya Sera ya Kilimo na Biashara nchini Marekani, Bi. Alissa Hamilton J. D (PhD), ameelezea kwa undani jinsi juisi ya machungwa inavyotengenezwa kiwandani. Undani huo umo kwenye kitabu chake cha; ‘Squeezed: What You Don’t Know About Orange Juice’. (Kitu usichokijua kuhusu juisi ya machungwa).
Katika kitabu hicho, mwanadada huyo anasema kuwa ni muhimu kila binadamu kujua kwa undani jinsi chakula chake kinavyoandaliwa, kwa sababu maelezo au lebo inayowekwa kwenye boksi, siyo tu haisemi ukweli, bali pia hailezi ukweli wote.
Anasema kwamba, kama kweli ‘pure orange juice’ tunayokunywa ilipatikana baada ya kukamuliwa chungwa peke yake na kuwekwa kwenye boksi, basi bila shaka ladha ingekuwa tofauti kati ya boksi moja na lingine, kwa sababu chungwa moja linatofautiana ladha na chungwa lingine. – mengine matamu, mengine makali.
Mbali na hilo, kila kampuni inayotengeneza juisi ya machungwa ina ladha yake. Juisi ya machungwa inayotengenezwa na kampuni ya Tropicana ina ladha tofauti na juisi ya machungwa inayotengenezwa na kampuni ya Ceres, sababu ya tofauti hiyo inaacha maswali mengi zaidi kuliko majibu.
Itaendelea wiki ijayo.
Chanzo:Global Publishers
No comments:
Post a Comment