ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 25, 2011

Kwa mara Nyingine tena "Anna Lukindo" afanya kweli kweli Uingereza!!!

 Anna Lukindo (katikati0 akiwa na Mariam Kilumanga(kulia) pamoja na mamodo wake.
 catwalk ikiendela
 design tofauti ya Annaluks
 Jestina akifanya vitu vyake
 Jestina Akifanyiwa mambo ya make up!.
 Jestina kwenye catwalk
 mambo ya catwalk yakiendelea
model akionyesha nguo za Anna 
 model akiwa mzigoni

wadau waliokuja kumpa sapoti Anna
URBAN PULSE ikishirikiana na Miss Jestina Blog inakuletea matukio katika picha ya Mtanzania mbunifu wa kimataifa Anna Lukindo 
(anaetumia  jina la Anna Luks) alipoonyesha mavazi yake ya kibunifu mjini London. 

Maonyesho hayo ambayo yalifanyika Ijumaa tarehe 19 Agosti 2011 Chelsea Old Town Hall, King's Road, Chelsea London. SW3 5EE. 
Maonyesho hayo  yalienda sambamba na kusheherekea siku ya Ubinadamu duniani.

Anna ameonyesha ubunifu wake wa kipekee  wa kutumia vitambaa asilia mfano gunia, kamba za katani na nyuzi mbalimbali ambazo anatumia ufundi maalum na kutengeneza vitambaa vyake mwenyewe. Wadau kadhaa kutoka katika nyanja tofauti walijitokeza kwa wingi kumuunga mkono na kuvutiwa zaidi kwa  kazi zake. 

Maonyesho haya yalitayarishwa na Mdoe ambaye ni Mkurugenzi   Wa uchaguzi husika wa wasanii wenye vipaji vya maigizo jijini London. Mbali na shughuli nyingine za kidiplomasia yalikuwepo pia mashindano ya kutafuta mshindi wa Tuzo ya Uso wa mwaka 2012 yaliyoongozwa na mwonyeshaji urembo na mwanamichezo Rachel Christie. Baadaye yalifuatia maonyesho mawili ya mavazi "back to back" yaliyofanywa na wabunifu wawili wa mitindo Anna Lukindo wa Anna Luks na "Adopted Culture" msanifu wa rangi, Nana Antwi.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Anna kwa kutembelea tovuti yake hapo chini
http://annaluks.blogspot.com/
Twitter:@AnnaLukindo

ASANTENI,

URBAN PULSE CREATIVE Akishirikiana na Miss Jestina Blog


No comments: