Familia ya marehemu Macrina Samaka wakijumuika pamoja katika misa ya kumuaga mpendwa wao iliyofanyikia Kanisa Katoliki la Masimbazi Center kutoka kushoto ni Dr Josephine Samaka, Jayden ( mtoto wa Dr Samaka), Juliet, Jonathan anajulikana kwa jina la JJ (mtoto wa Claudia), Claudia na Clara.
Pandri akiongoza misa na kutoka kulia ni Mr Joseph Samaka(baba wa marehemu), wapili kushoto ni Francis na Anthony (kaka zake marehemu)
Hapa ni ndugu wa karibu wa marehemu wakiwa wamebeba msalaba uliosimikwa juu ya nyumba ya milele ya Macrina Samaka Francis aliyebeba msalaba na Anthony aliyebeba picha ya marehemu dada
Familia ya Macrina Samaka,ndugu,jamaa na marafiki wakiwa kanisani wakifuatilia misa kutoka kulia ni Mrs Mahinga, Mrs Chagula, Mrs Samaka (mama wa marehemu) na Mr Samaka (baba wa marehemu), siti ya nyuma kutoka kulia ni JJ, Juliet, Jayden na Dr Josephine Samaka.
Ndugu,jamaa na marafiki wakifuatilia misa
Familia ya Marehemu ikipiga picha ya pamoja mbele ya nyumba ya milele ya mpendwa wao Macrina Samaka
Shukurani Toka Kwa Familia Ya Joseph F. Samaka
Familia ya Bwana Joseph Samaka inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walio shiriki kwa namna moja au nyingine katika kusafirisha mwili wa mpendwa wao marehemu Macrina Samaka, na kuwezesha mazishi yake.
Ni vigumu kumtaja kila mmoja, ila tungependa kutoa shukrani za pekee kwa Jumuiya ya Watanzania walioko Marekani, na vile vile kwa Ubalozi wa Tanzania ulioko Washington DC.
Shukrani zingine ziende kwa jamaa na marafiki walioko nchini Tanzania.
Hakuna cha kuwalipa, bali Mungu awabariki na awazidishie pale mlipotoa.
Mungu ailaze roho ya marehemu Macrina mahali pema peponi.
Bwana Alitoa na Bwana Alitwaa, Jina La Bwana Lihimidiwe
Amen
No comments:
Post a Comment