ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 13, 2011

Neno la Shukurani

Kwa niaba ya Kamati iliyokuwa ikiratibu ukusanyaji wa michango na Mipango
ya  kusafirishwa mwili wa Marehemu Macrina Samaka kwenda Tanzania kwa
mazishi,tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Watanzania na watu wote
waliokuwa bega kwa bega pamoja nasi katika kufanikisha shughuli hii.
Aidha, tunamuomba dada yetu Juliet Samaka atufikishie salamu zetu za
rambirambi kwa wazazi Ndugu na jamaa wa marehemu walioko Nchini Tanzania
mara atakapofika huko.Tutaendelea kuungana nanyi katika sala zetu, ili
ndugu yetu Macrina aweze kupata mapumziko yake ya milele kwa Amani Amina!
Kwa watanzania tuliobaki hapa Marekani tunawaombeni kuendelea na moyo wa
kuungana na kusimama kama kitu kimoja katika kushughulikia mambo mazito
kama haya kila yanapotokea.
Hakuna anayejua nani atakayefuatia,ninaweza kuwa ni mimi,wewe au yeyote
kati yetu.Hili ni jambo linalomuhusu kila mmoja wetu.Kwa maana hiyo,
inatupasa kuendelea kushirikiana bila kuchoka ili kuonyesha umoja wetu
katika misiba inayotupata tukiwa huku ugenini.
Tunawashukuru sana kwa kuhudhururia tukio hili la kutoa heshima za mwisho
kwa marehemu, mwenyezi Mungu awabariki.

Mwili wa Marehemu utaondoka Jumatano na unatarajiwa kufika Tanzania Ijumaa.Kwa haya machache tunasema Asanteni
sana!

Juu na chini ni Jeneza la mwili wa Marehemu Macrina Samaka likiingizwa Kanisani St Camillus,iliyopo Silver Spring,Maryland ambako ndipo palisaliwa sala ya kumuaga Dada,Rafiki,mfanyakazi,na Mtanzania mwenzetu kwa Safari yake ya Tanzania kwenye nyumba yake ya milele.
Rafiki wapenzi wa Marehemu tangia nyumbani Tanzania,Suzie(shoto) na Juliana wote wametokea Boston(MA)
kutoka shoto ni Juliana,Suzie,mdogo wa marehemu,Juliet,Wahida na Natasha(mtoto wa Wahida)
Click Read More For all Church Photos

8 comments:

Anonymous said...

jamani misiba ya siku hizi hamna kulia watu wanaweka smile nzuri kwenye picha lol tumesahau mila zetu

Anonymous said...

Jamani poleni sana!!!kwani hio ndio nnjia ya kila Mja ktk hii Dunia, na tunapolia, tunalia mazoea!kumbuka kila moja wetu nnjia ndio hio,nasema poleni sana ndugu zangu wa Tz Mungu awabariki nyote.

Mzee wa Changamoto said...

Shukrani kwa wote waliofika kutuwakilisha na shukrani kwako kutushirikisha
Bless

Anonymous said...

Hii inatufanya binadamu sanasana wapenda mashauzi kuwaza Mara mbili mbili Kama huyu dada amechukuwa good deeds tu huko alipoenda hamna cha gucci nyumba nguo wala mashauzi ya aina yeyote.
Anyway this is a wake up call wajameni tutende mema yatakayo tuletea dhwawabu kaburini na judgement day,si wakristo Buda Indu au Muslims.

Anonymous said...

you will be dance with angels now
walking in new life

Anonymous said...

poleni sana wote mlofikwa na msiba huu, Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani.

Anonymous said...

Sisi tulimpenda lakin mwenyezi mungu alimpenda zaidi akamchukua. Amen

Anonymous said...

Rest well. I was there. Love u. I remember friend of mine were til the last minute. Hugs n kisses again. Lv u sis in law.