ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 7, 2011


TUISHI KWA KUJIFUNZA

Ndugu zangu wa ughaibuni,
Maisha ni safari ndefu sote hatujui hatma zetu kimaisha . Ni wajibu wetu sisi kama Watanzania kukumbushana historia yetu kama Watanzania sote ni ndugu; si wa kuzaliwa bali mahusiano yetu kama Watanzania.

Watanzania wenzangu wa maeneo ya Washington DC na vitongoji vyake mtakubaliana nami mahusiano yaliyokuwapo miaka ya nyuma tuliishi na wengi miongoni mwetu bado tunaendelea kuishi kindugu,ni ukweli usiopingika wengi wetu huku hatuna ndugu wa damu, undugu ni wa kirafiki na ujamaa na Utanzania tuliokua nao.

Miaka ya hivi karibuni umezuka msemo hapa Metropolitan DC WATANZANIA HAWANA MPANGO! Nakubaliana na wote wenye hisia hizo. Cha kushangaza miaka yote hao WATANZANIA WASIO NA MPANGO ndio wamekuwa mstari wa mbele kwenye kusaidia panapotokea shida mbalimbali. 

Tumekuwa tukisaidiana bila kujali imani zetu kidini wala itikadi zetu kisiasa. Wapo wachache miongoni mwetu wenye dhana potofu kuwa Watanzania nuksi na wameamua kujitenga na jamii, Binadamu wote tuna mapungufu na migongano siku zote itakuwapo. 

Nawakumbusha tu wenye dhana potofu labda wamesahau tumetoka wapi,naamini Watanzania ni watu wenye ukarimu na upendo na wenye kusamehe. Ipo mifano ya matukio mengi tu yaliyowahi kutokea hapa DC yanathibitisha maneno yangu sina haja ya kuyakumbusha. 

Ndugu zangu nyie mlioamua kutojichanganya na hawa mnaosema nuksi wa Kitanzania fikirieni tena. Sisemi muwe na urafiki wa kutembeleana majumbani la hasha! Ninachosema mjitokeze angalau jamii ya Watanzania wenzenu iwajue. 

Na inapotokea shida kama msiba,naomba tuwe kitu kimoja,tunaweza kuzaliwa tumbo moja lakini si lazima tuwe marafiki na inapotokea umepatwa na shida mimi ndio nitakuwa wa kwanza kufika kwa sababu tumechangia damu na sisi tuishio mbali na nyumbani,Utanzania ndio damu yetu.

Sasa hivi hakuna jumuiya ya Watanzania DC hiyo haikuzuii kujuana na Watanzania wenzako,tunazo jumuia za kidini, yapo makanisa ya Watanzania, ipo jumuiya ya kiislamu. Ni aibu inapotokea shida au msiba huwezi kufika hata kwenye msiba kwa sababu Mtanzania huyu hakuna anayemjua na unaposikia eti alikuwepo hapa miaka mingi,tena ni jirani yako mlango wa pili,hapo ndio kabisa hata simu hutopiga. 

Kama uliweza kuishi na Watanzania milioni 40 utashindwa vipi na Watanzania ambao hata idadi yao haizidi hata 500? Maisha ni kupanga, na kupanga ni kuchagua nawausia chagueni njia iliosahihi.

Mtu apoamua kuishi peke yake sio kweli amejitenga au kuukana Utanzania,hayo ni maisha yake,naomba usimuadhibu anapopatwa na shida bado ni Mtanznaia na itaendelea kuwa hivyo mpaka mwisho wa maisha yake.

UMOJA NI NGUVU,UTENGANO NI UDHAIFU

ASANTE

Huu ni waraka wa Mtanzania kwa Watanzania kupitia VIJIMAMBO!

28 comments:

Anonymous said...

Dj Luke: Naomba kutoa maoni yangu kuhusu huyu aiyeandika habari hii.
Kuna ukweli katika maandishi yake ila naona sehemu kubwa ameandika kwa hisia na akiwa na lengo maalumu. Pia naona ameshindwa kufanya utafiti wa kina na amejichangaya ( contradiction) kwenye hoja yake.
Ameeanza vizuri kuhubiria upendo na mshikamano tuishi kama wandugu kama ilivyo mila zetu. Katika aya ya tatu kutoka chini naamini kabisa anamzungumzia marehemu ama msiba uliopo sasa DMV kwa lengo la kufikisha ujumbe wake mahususi kwa walengwa fulani fulani. Je alifanya utafiti kujua kama Marehemu labda ndo hakutaka kuishi na watu? maana amesema "alikuwa jirani ya fulani next door, na fulani kujua kwamba alikuwa jirani yake mlango wa pili, ndo hata simu hapigi" Je Marehemeu alitaka kujulikana kama mtanzania ama? Binafsi sijui ni muda gani amekaa hapa DMV ila nimehudhuria, Misiba mingi mno, harusi, Babyshower, Idi pamoja na mikusanyiko mingine mingi ya watanzania, sijawahi kumuona wala kusikia hilo jina hadi pale ulipotutangazia habari za msiba huu. Naelewa tuko wengi hapa kwa sasa na wengine wana makundi yao ya kusaidia, ambayo ni sawa kabisa, sasa unaweza kutupa labda historia zaidi.Najua hapa tunatafuta njia ya kusovle hili tatizo, ila ni ukweli mtu una choice ya kuchagua lifestyle yoyote ila lazima pia ukubali kulipa gharama yake, bila kubugudhi au kwa gharama ya wengine/wanajumuia. Kingine, mtoa hoja, katika aya ya mwisho, anasema" na mtu anapoamua kuishi peke yake siyo sawa kama amejitenga na watanzania", sasa sijaelewa hii aya ina maana gani kama siyo kujichanganya na hiyo ya tatu juu na kupoteza maana ya ujumbe wake wote. Mi nasema tusitumie emotional/hisia kwenye hili;ndiyo msiba na kwa kila mtu,lakini itumike busara, balance na uwazi na iwe somo kwa wote na siyo kumobolize watu kwa kutumia hisia maana yatajirudia tena na tena ma tutaona ndo desturi hii.
Kingine, Msiba huu ulipotokea, bwana luke uliweka picha pamoja na barua na kutoka kazini kwa muhusika ikiwa imesainiwa na mkurugenzi wake wa kazi, akiwa anasikitika kutangaza kifo hiki pamoja na kwenda mbali zaidi na kusema nanukuu "kampuni inafanya utaratibu wa mazishi, na siku ya maomboleza watafunga ofisi kutokana na mchango na heshima ya marehemu" mwisho wa kunukuu..
Nilijaribu kuifuatilia kampuni hii na kugundua ni kubwa kiasi kiuwezo na pia marehemu alikuwa anafanya kazi kama accountant na katika website ya kampuni ni majina manne tuu ya maofisa wa kampuni walikuwa listed na la marehemu likiwa moja wapo. Sina uhakika ila naamini kwa level aliyofikia marehemu, je hakuna life insurance kutoka kazini kwake au mchango wowote unaoweza kutoka kwa muajiri wake? Naona hili sijalisikia, sasa Bwana Luke je hao wana kamati wanaweza kutueleza wanajumuiya wamefikia wapi kwenye hili. Inawezekana kabisa marehemu alishajiandaa na ningeoomba muangalia kama kuna insurance au chochote kutoka kwa muajiri wake ili kufanikisha kwa haraka zaidi safari yake ya mwisho kuliko anavyoendelea kupigwa na baridi kama uliyosema katika matangazo yako mengine. Mwisho pia kuna suala la credibility kwa baadhi ya wanakamati pia liangaliwe. lazima liwekwe wazi. Saa nyingine siyo kwamba watanzania hawataki kuchanga, bali pia inawezekana kuna tatizo katika baadhi ya hao wanaopokea michango mbele ya jamii kutokana na historia ya huko nyuma. Watanzania wa leo siyo wale wa zamani wa kusahau na mifano ipo hapa hapa DMV.
Mwisho nawaomba watanzania wenzangu popote pale tulipo hapa DMV leo tujitokeze kwa wengi kuweza kufanikisha safari ya mwisho ya dada yetu, na kama alivyosema DJ Luke, safari hii ni ya kila mtu na hatujui lini itakuja kwetu. Nawaombeni radhi wadau kama nitakua nimechafua hali ya hewa kwa maoni yangu.

Anonymous said...

Dj Luke, sikuwa na lengo la kuleta malumbano ndani ya jamii.Ujumbe lengo lake ni kukumbushana kama watanzania. Ndio maana nilisisitiza hatuna ulazima wa kuwa na urafiki wa kutembeleana majumbani bali tujuane tu hata kwa majina inatosha, unakaa wapi unafanya kazi wapi hayo si muhimu. Muhimu jitokeze jamii ikujue hilo ndio lengo la ujumbe.

Anonymous said...

Wengine hawajichanganyi sio kwavile hawapendi, ila schedule zinakuwa zimepamba moto. Kazi mbili au tatu jamani muda wa kujichanganya inakuwa ngumu.

Anonymous said...

Si kwamba kila mtu ambaye hajichanganyi anaringa lahasha,na kwa kweli wengi wetu wamekuwa ni "victim" wa mikusanyiko hiyo na ukweli unabaki pale pale kuwa watanzania wengi hawapendi kujichanganya kwa sababu wamechoshwa na majungu,kutokuheshimiana,ulevi wa kupindukia,fujo,kupigana na ukosefu wa nidhamu wa baadhi yetu katika mikusanyiko hiyo.

Anonymous said...

hiyo message mbona inachanganya. mara unahimiza wa-TZ tuwe na mshikamano, then mwisho unasema mtu anapoamua kujitenga na wa-TZ its ok, so which is which? like mdau alivyo-comment hapo juu, unapoamua kuji-isolate then buy life insurance thats the isolation cost au?

let me tell u why wa-TZ tunaamua ku-mind our own businesses, kikubwa ni tuna-avoid majungu na kupokonywa waume/wake zetu. mtu akishakujua au akishakuja kwako tu, basi atakuchunguza unaishi vipi ili apate kukusema kwa watu. watanzania tuko very quick ku-judge maisha ya watu personally i hate that.

lastly, hivi kwa nini watanzania USA hatununui life insurance. wengi wetu siku hizi tuna makaratasi and life insurance is less than $10 a month. na mtu anapotutoka tuwe tunacheki kwanza kama ana life insurance kabla ya kuanza michango. hiyo itaspeed up hizi process

Anonymous said...

iwi kuwe na mshikamano ni lazima watanzania wa DMV tupunguze majungu. hivi unadhani mtu ataamua kujitenga tu bila sababu? wewe mwandishi inabidi utafute whats behind the kujitenga kabla ya kutoa lawama.

Anonymous said...

Jamani mchango wa msiba kwa ajili ya shughuli za mazishi ni kitu gani? Ni Asilimia chache tu ya watu wanaotoa $ 100 kama mchango. Msiba una gharama nyingi especially unapofanyika kwa mtu. Michango ni kawaida na itazidi kuwa kawaida yetu watanzania bila kujali aina ya insurance mtu aliyonayo.
Cha kujifunza ni kuwa kama mwanadamu kila mtu anastaili hesima zake za mwisho na ukizingatia kila mtu atakufa, na tutengeneze njia nyoofu. Mtu asijitenge kiuzungu na atake kuzikwa na kuagwa kibongo. Kaa ufikiri wengi wetu sasa tumefika 30's na zaidi limbukeni wa Maree Marekani na abaki hivyo hivyo.
Pesa haimpi mtu utu!
Kwa hayo na tuache tofauti zetu na tuungane!
Ninajivunia Wanaashington nilipopatwa na Msiba walinisaidia na kunifariji sana. Mbarikiwe!

Anonymous said...

majungu hayakosi jamiini, tuungane tu tumsindikize mwenzetu. Nafikiri wengi watakuwa wamepata picha halisi sasa!

"Wake up Washington DC"

Anonymous said...

Asante mwana blog hapo umesema! Na tuungane sisi wote ni ndugu.

Anonymous said...

Narudia tena, majungu, fitina, uwongo umbeya ni vitu vya kawaida ndani ya jamii. Hivyo havikwepeki si hapa wala huko nyumbani.Tunajaribu kukwepa ukweli lakini hii ndio hali halisi jamani tujuane tu hata kwa majina. Narudia tena tujitokeze tujuane hata kwa majina. Hatuna ulazima wa kukaribishana majumbani; tunaweza kujuana kupitia taasisi zetu za kidini cha msingi tujitokeze. Ni rahisi kusema mengi kama halijakukuta. Ukweli tunaujua tusilete malumbanao ambayo hayana mwelekeo. Tunachojaribu ni kuleta mshikamano na si vinginevyo. Tafakari kabla hujanena!

Anonymous said...

Mdau unayeongelea life Insurance nakubaliana na wewe. Hata ukiwa na life insurance si inabidi wawepo watu wa kuratibu sasa kama tutajificha hiyo life insurance itafanyakazi peke yake? Ukweli life insurance ni supplement tu kila itavyokuwa utahitaji watanzania wenzako.Hatuna haja ya kuogopana hatujafikia kuwa na sifa ya wanyama. Upendo wetu na ukarimu upo palepale sisi ni watanzania.

profa said...

Wote waliochagia wamenigusa kwa namna moja au nyingine.Kama mzazi anapokuwa na watoto wasio na tabia nzuri na wenye tabia nzuri na bado hawatengi na anawaona wote kama watoto wake,ndivyo mama yetu Tanzania ilivyotulea na ndivyo tunapashwa kuenenda hata kama tuko nje ya mipaka ya nchi yetu.Kuna wengine wanapata nafasi ya kuhudhulia msiba kama huu na wengine hawatapata kutokana na mfuko,au muda wenyewe nao bado ni watanzania na tunawapenda bado.Tusianze kuwajaji visivyo bila kujua ni nini kinawasibu.
Mimi nina tatizwa na jambo hili la party za kila mara.Siwazuii wanaoamua kujifurahisha au kusheherekea majumbani kwao baada ya mafanikio fulani,bali hawa wanao enda kwenye party za wengine bila hata kuitwa au kualikwa.Jamani ndiyo utanzania huo?kwa nyumbani vijijini jambo hili ni sawa kwa baadhi ya makabila lakini hapa amerika ambako hata maji ya kunawa ni bill lukuki? na wengine wanazitumia party hizi kama stage ya kuwajaji wengine eti hawajichanganyi ebu tujiunge katika jamii staarabu tafadhali

Anonymous said...

Maoni yote ni ya busara, cha muhimu ni kuishi na kufanya kilichotuleta huku USA, acha mtu aishi anavyotaka na panapokuwa na shida let people wajitolee kwa moyo kwani maisha ni magumu na kutupiana lawama siyo jambo la busara. Wenye tabia za majungu wanajijua na hii ni fundisho kuwa they have to stop kwani wanawakosesha misaada watu wengine, kwa hiyo jitahidi kufumba mdomo kwa lolote utakalo likuta kwa mtu au kama unaona utatoa comment za uongo basi don't go there or don't be involve in any group. Hii itasaidia sana, mtu ukiona mwelekeo wa mwenzio hauendani na mambo yako au mwisho wake unaweza kuwa fujo, jitaidi kumtoa huyo mtu kwenye maisha yako as soon as possible, there is no high standard or high profile hapa, ni jinsi watu wanavyojisikia au wanavyojiona lakini tukumbuke MR KIFO haaangalii what you have or don't have akiamua kuja anakuja bila hodi MEN.
BE GOOD AND LIVE YOUR LIFE AND STOP MAJUNGU'S NA KUJIONA ONA NA KUJIDAI DAI. MAISHA HAPA EVERY BODY CAN MAKE IT NI KAZI KWA MBELE REGARDLESS KAZI GANI UNAFANYA DOESN'T MATTER WHAT MATTERS IS ARE YOU MAKING DOLLARS.

Anonymous said...

Kaka Luka Mungu akujaalie kwa kupitia blog hii ya moyoni yanatolewa.Mimi binafsi nimejifunza mengi.
Asante sana.

Anonymous said...

nilijitenga sababu naogopa kuibiwa mke wangu kwa mara ya tena. kijana wa kitanzania alininyang'anya tonge mdomoni hivi hivi najiona, tena wa hapa hapa DMV. sina hamu. watu heshimuni wake/waume za watu!

Anonymous said...

Kweli mengi yameandikwa na yataendelea kuandikwa, ni ukweli usiofichika kwamba sisi watanzania tulio wengi hapa DC tunakwenda misibani kwa makundi na majina. Kweli inachosha na kusikitisha sana pale ambapo wewe ukisikia kila msiba wa mtanzania unakwenda hujali kama unamfahamu au humfahamu as long as ni mtanzania mwengio inamaana ni ndugu yako. Lakini wewe Msiba ukifika kwako huoni mtu, unalia peke yako. Kweli utaacha kujitenga na watu?? Jamani tubadilike ndugu zangu watanzania kwani kila mtu atakufa au kufiwa kwa muda aliopangiwa na Mweyezi mungu, just a matter of time; ukweli utabakia pale pale kwamba KIFO AKINA HURUMA na kila nafsi itaonja mauti. Tunapo patwa na Msiba tafadhalini ndugu zangu watanzania tuwe kitu kimoja, tuchangiane na kufarijiana.
Pendekezo: kulingana na wingi wetu sisi watanzania especially hapa DC tunapofikwa na msiba tuungane na tujumuike. Nadhani watanzania tuishio DMV tunafika watu 1,000 (makisio yangu)Mfano kila mmoja wetu akishiriki na kutoa $10 or $20 tu kweli inatosha sana watanzania wenzangu. Tushirikiane tujumuike jamani tunamchukiza hata Muumba wetu wapendwa.

Anonymous said...

Watanzania wenzangu jamani tuache makundi ya maneno, kujitenga na kwenda misibani kwa majina, majungu na fitina tushirikiane ndugu zangu. Angalieni wenzetu wa magaribi wanavyoshirkiana kwenye matatizo ya kila aina. Sisi tunakalia majungu na ugomvi wa uchonganishi jamani. Lazima watu wasiopenda makuu wajitenge.

Anonymous said...

kaka pole kwa kupoteza tonge mdomoni. Hiyo isiwe sababu ya kujitenga na jamii. Huyo uliyempoteza haikuwa riziki yako. Nina uhakika uliye naye sasa ndiyo andiko lako. Uliye mpoteza hakuwa na mapenzi na wewe alitafuta sababu; usiogope watanzania bado sisi ni nduguzo.

Anonymous said...

Kaka unayeongelea party napingana kidogo na mawazo yako. Party ni starehe ni jambo la hiyari siamini kama kutohudhuria party ni kujitenga; binafsi sijawahi kuhudhuria party za get together; sherehe ninazohudhuria ni nimekaribishwa na ndugu na jamaa. Hapa tunaongelea mambo ya msingi ambayo wote yanatugusa. Hilo la party lisikutishe tujumuike kwenye mambo ya msingi.

Anonymous said...

Ndugu yangu unayeongelea schedule nakubaliana na wewe. Labda tu nikuulize katika siku 365 unafanya kazi siku zote? Najua majukumu ni mengi sana lakini naomba ujitahidi angalau tafuta wasaa wa kuwasiliana na kujuana na watanzania wenzako.

Anonymous said...

wengine haoooooo...wanakurupuka kuandika hata bila kusoma comment za wenzao vizuri.Mimi niliye muelewa huyo kaka kuhusu party anamaanisha kwamba tusiwe tunadandia party za watu ovyo ovyo na hata mie inanikela maana mtu anadiliki kwenda phili kwenye b,day ya mtu tu kisha anaanza kuomba ride kwa watu namna ya kurudi.
Pia huyo kaka anasema tusitumie hizo party mshenzi kuwajaji wenzao kwamba hawajichanganyi.Hapa point ni kuhusu kuwa pamoja kwa watanzania wewe dada..siyo kwamba point ya jamaa haina mantiki.

Anonymous said...

kweli makundi siyo mazuri. nimegundua DMV kuna makundi kama ifuatavyo.
1. Watu walitoka masaki na oysterbay
2. watu waliotoka uswahilini
3. wazanzibari na wapemba
4. wa mikoani AKA washamba, AKA walipita Dar transit kuchukua visa

ukienda kwenye shughuli za wa masaki humkuti mpemba wala wa uswahilini, ukienda kwenye shughuli za wapemba huwakuti wabara nk. hivyo ndivyo ilivyo hapo DMV. na wanaojitega wengi ni wa mikoani sababu they don't fit anywhere kwenye hizo communities za Dar. so change is needed

Anonymous said...

Kujitenga kwa watanzania kuna mengi, niliwahi kushuhudia sehemu fulani watanzania wamekusanyika kwa kusaidiana. Mara inaonekana hivyo vikundi vya ajabu ajabu vikatuma mtu mmoja mjinga mjinga hivi aanzishe vurugu za matusi zilizopelekea umwagaji damu shughulini. Je, huo ni ungwana watanzania? Aliyefikwa atapata hamu kweli ya kujichanganya na watanzania tena?? ndugu zangu watanzania tuache chuki binafsi,tupendane na tushirikiane tubadilike

Anonymous said...

Mimi nimetokea Oysterbay lkn mbona ninashiriki shughuli zote jamani? kweli wapo baadhi yetu wa Masaki Oysterbay wana-act; kama wao wanamaana sana kuliko watanzania wengine wowote, mbona nao wanafanya kazi hizi hizi tu? Basi waingie maofisi makubwa kama wanaweza ili tofauti ionekane basi...lol acheni majungu na fitina za ajabu...kwa wale ma expert wa makundi unatakiwa kujua kwamba. UMOJA NI NGUVU NA UTENGAO NI UDHAIFU...HESHIMA NI KITU CHA BURE...Acheni kuwasengenya wenzenu sijui huyo wa mikoani, mara huyu wa manzese. Kila mtu ameingia marekani kivyake na ni imani yangu kwamba binadamu wote ni sawa mtu akikutreat vizuri wewe utamtreat vizuri zaidi na akivanya tofauti nawewe utatreat the same. To me Oysterbay, masaki, mburahati, gongo la mboto, vingunguti, mikoani, wapemba na unguja wote ni viumbe vya Mungu na tunathamani mbele yako wote. mwenyezi Mungu akubagua mtu ndo maana wote tupo hapa marekani. tushirikiane

Anonymous said...

mie wa mikoani, but napendelea kwenda kwenye shughuli za wapemba na wazanzibari maana kule kuna mahanjumati ya ukweli. huko kwa ma masaki na oysterbay utaambulia wali mkavu bila mchuzi....mnabisha?

Anonymous said...

seriosly, embu tuache huu u-masaki sijui oysterbay tuungane tuwe kitu kimoja. nime-realize sisi wa mbagala na vingunguti, mikoani etc tuna maendeleo kuliko mbona, so where u from doesn't determine where u go....so kama mdau hapo juu alivyosema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. so lets forget about all these mikoani sijui nini BS tuungane tusaidiane kutoana stress za maisha jamani!

Anonymous said...

Tumechangia mengi sana yenye kutia moyo tunachohitaji ni umoja, lazima tukubali tuwe na pa kuanzia. Watanzania wenzangu jumamosi saa tano asubuhi tujitokeze kwa wingi tumuage marehemu; binafsi sikuwahi kumfahamu Macrina nimeshachukua day off. Wale wa Osterbay, Vingunguti wote tupo safari moja. Dj Luke naomba yakiisha mambo ya msiba uratibu kitu ili watanzania tufahamiane. Kujuana ndio mwazo wa kuheshimiana.

Anonymous said...

jamani wabongo aibu tupu bado tuna mambo ya ujima hivi siku hizi kuna mambo ya masaki ,oster na kwa matola?nadhani siku hizi ni pesa yako tu na akili yako hata ukiwa unaishi wapi ukitaka maisha yako yawe poa ni bidii hao wamasaki mbona wanaangaika tu humu mjini jamani bado wanafikia kwa mama la muhimu ni kueshimiana na upendo,na tenda wema uende zako ukigonja shukrani utakwaana na kila mtu kuna watu wanapenda kufanyiwa tu siyo wao wafanye laaaasha mwiko kwao