Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na baadhi ya Viongozi, kubeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja jana.
Waziri Mstaafu, Edward Lowassa, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa maziko yaliyofanyika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya kati Unguja jana.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa maziko yaliyofanyika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya kati Unguja jana.
Mwenyekiti wa Makati ya Bunge ya kudumu ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa maziko yaliyofanyika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya kati Unguja jana.

Rais wa Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim Seif na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Mbunge wa Bumbuli na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, January Makamba wakiwa katika shughuli ya maziko ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Silima. Maziko hayo yamefanyika jana Agosti 24 katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja.
Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais


No comments:
Post a Comment