Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed,
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imelitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaokula hadharani na kuvaa nguofupi wakati huu wa mfungo mtukufu wa Ramadhani.
Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, alipozungumza na waandishi wa habari jana.
Alisema serikali imeamua kutoa agizo hilo baada ya kujitokeza baadhi ya watu kuonekana wakila mchana hadharani na baadhi ya vijana kuonekana wakiwa wamelewa na kuranda mitaani kinyume na misingi ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Aidha, alisema baadhi ya wanawake wamekuwa wakionekana mitaani wakiwa wamevaa nguo zisizokuwa na heshima.
Waziri Aboud amesema kwamba baadhi ya migahawa na nyumba za kulala wageni zimekuwa zikitoa huduma mchana katika kipindi cha Mwezi Mtukufu. Waziri Aboud alisema kimsingi wananchi hawazuiwi kula mchana kulingana na imani zao, lakini wanatakiwa kufanya hivyo wakiwa katika maeneo ya faragha kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawataka wale wote wanaojishirikisha na vitendo hivyo waache mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria pamoja na kwenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na mafundisho yake Mtume Mohammad,” alisema.
Aidha, alisema serikali inatarajia wananchi wote Unguja na Pemba watashirikiana kurudisha heshima ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
Waziri Aboud amesema serikali imeamua kutoa tamko hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka Jumuiya moja ya kidini Zanzibar juu ya kuwepo watu wanaokula mchana na kuvaa nguo fupi bila kuzingatia misingi ya mfungo wa Mwezi wa Ramadhani.
CHANZO: NIPASHE
2 comments:
Ijapo kuwa mie ni mkristo, ninamuunga mkono Mhe: Waziri kwa hilo watu wanatakiwa kuwa na nidhamu na kuheshimu imani ya dini za wengine. Kwani ustarabu ni kitu kinachopendeza kila mwenye fikra sahihi.
sIYO HAKI HATA KIDOGO, UNAPOSEMA WANAKULA HADHARANI UMAMAANISHA NINI, NA IKIWA ATAFUNGIA MIGAHAWA YOTE JE WALE WASIOFUNGA WATAKULA WAPI, NAHATA WAISILUMU WENGINE WASIOFUNGA PIA UHITAJI KULA JE? WAO WATAKULA WAPI? HAYA MASWALA YA UDINI NAKUJIFIKIRIA WAO TU,UPUUZI MTUPU.
FUNGA KULA KAMA UNAPENDA IWE NI KWA MAPENZI YAKO AU KWA IMANI ZAKO ISIWE LAZIMA KWA KILA MTU ETI KWA KUWA WEWE UMEFUNGA.
HUU NI UDINI,ZANZIRA SIYO ISLAMIC STATE HIVYO MATAMSHI KAMA HAYO HAYPASWI KUUNGWA MKONO HATA KAMA YEYE NI KIONGOZI.
NI MPUUZI NA MAWAZO YAKE YA KIPUUZI.HATA KAMA MIMI NI MUISILUMU SILAZIMISHWI KUFUNGA HYO NI IMANI YANGU, ILIMRADI SIMSHAWISHI MTU YEYOTE KUNIFUATA NIACHWE NILE,NINYE NI LALE. YEYE NANI MPAKA ATOE MATANGAZO HAYO,SIYO SHEHE SASA KIVIPI KIONGOZI WA SERIKALI ATOE MATAMSHI YA JUMLA JUMLA ETI WANOKULA OVYO,YEYE NDO MLA OVYO,ANAKULA USIKU KUCHA OVYO KUTWA NZIMA ANAKUNYA NA KUTUJAMBIA OFISINI KISHA ANAWAAMBIA WENGINE WALA OVYO MPYUUZI MKUBWA.
Post a Comment