Waziri Afya na Ustawi ya Jamii, Dk.Hadji Mponda
Serikali imezuia kuuzwa kwa samaki walioagizwa kutoka Japan na kuamuru uchunguzi ufanyike ili kubaini samaki hao kamawameathiriwana mionzi ya nyklia.
Hayo yamesemwa jana na Waziri Afya na Ustawi ya Jamii, Dk.Hadji Mponda, baada ya kukagua maghalaya kuhifadhia samaki ya Kampuni ya Alpha Crist iliyopo eneo la Kipawa, jijini Dar es Salaam.
Kampuni hiyo inadaiwakuingiza nchini kontena tano zenye uzito wa tani 25 kilamoja za samaki aina ya kamongo wiki tatu zilizopita kutoka nchini Japan na kuzusha hofu ya kuwepo na mionzi hiyo hatari.
Akizungumzana NIPASHE, Mponda alisema Serikali imefanikiwa kukusanya sehemu kubwa ya samaki ambao walikuwa wamesambazwanchini kwa ajili ya kuuzwa na kuwaweka katika uangalizi maalum.
Alisema, wakati shehena hiyo imezuiawa,hatua mbalimbali zinafanyika ikiwa pamoja na kufanya uchungizi wa kimaabara kuona samaki hao wapo salama kwawalaji.
“Serikali ina wasiwasi na samaki hawa waliotoka Japan,tumeamua kuwazuia wasiuzwe na shehena zote zilizopelekwa mikoani tumezirudisha,” alisema waziriMponda.
Alisema wataalamu kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wameanza kuangalia sampuli ya samaki hao kabla ya Serikali kutoa tamko.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ganesh Vedgir alisema anaamini samaki hao wapo salama kwa sababu wamehakikiwa na idara zote za kuangalia usalamawa chakula za hapa nchini na nchini Japan.
Alisema kabla ya kuingizwa nchini alipeleka sampuli TFDA na kukubaliwa samaki hao ni salama na wanafaa kuliwa na watu.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment