ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 27, 2011

Yanga matatani kwa kutovaa jezi Voda

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga, imeandikiwa barua na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kuwataka wajieleze ni kwa nini wamekataa kupokea jezi zilizotolewa na wadhamini wa ligi hiyo, kampuni ya huduma za simu ya Vodacom, imeelezwa.
Akizungumza jana, Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa shirikisho limefikia uamuzi wa kuitaka Yanga ijieleze kutokana na timu hiyo kushindwa kupokea na kutovaa jezi zenye nembo ya wadhamini hao katika mechi zao mbili za ligi walizocheza dhidi ya JKT Ruvu na Moro United kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Wambura alisema kwamba wanataka kujua ni kwa sababu zipi klabu hiyo imefikia maamuzi hayo na ndipo waweze kutoa maamuzi kutokana na kugomea jezi hizo.
Alisema kuwa klabu zote zinazoshiriki ligi hiyo zinatakiwa kufuata yote yaliyomo kwenye mkataba uliopo kati ya TFF na Vodacom na kuongeza kwamba ligi ni mali ya shirikisho hilo.
Alisema vilevile kuwa Yanga ambao wanadaiwa kuwa wameanza mazungumzo na makampuni mengine kwa ajili ya kusaka udhamini, inatakiwa kutotafuta mdhamini

CHANZO: NIPASHE

No comments: