Blogs katika nchi yetu ya Tanzania pamoja na sehemu nyingi duniani zimekuwa kiungo muhimu sana katika kuupasha umma habari. Alianza Michuzi kublog wakafuatia wengi na wengi wao wakiwa waandishi waliobobea na wasiobobea katika Nyanja ya habari Tanzania.
Nimesukumwa kuandika haya ya leo kutokana mwenendo wa bloggers wengi ambao kwa hakika unaelekea si tu kutukanisha taaluma ya habari, bali pia kuvunja maadili ya uandishi wa habari kwa ujumla. Blogs zina kusudi la kufikisha ujumbe kwa mtindo uleule ambao websites nyingine za habari kama cnn.com, bbcworld.com, ippmedia n.k zingefikisha ujumbe kwa jamii. Ni dhahiri kwamba kanuni na sheria za uandishi wa habari zinapaswa kuzingatiwa na wanablogu pia.
Tanzania tuna blogs nyingi ambazo zimepoteza mvuto hasa kwa sababu ya ama kuhamisha habari za wenzao au kuingia mikataba na wenzao ambayo inafanya zisiwe na jipya zaidi ya kuhamisha kila kitu kilichotolewa na wenzao. Imefika wakati ambao nadhani hata bloga anaweza kurusha habari za siku nzima akiwa chumbani kwake kwani teknolojia ya ‘copy & paste’ inamruhusu kufanya hivyo. Lakini ni kosa kubwa kwani wasomaji hutegemea mhabarishaji aliyejitolea kutoa habari kwa umma ajishughulishe kutafuta habari na sio kunakili mapicha na habari zilizoandikwa na bloga mwingine…. HII INABOA!
Nimeona blogs nyingi ziki post story na picha kwa namna ile ile kitu ambacho inaonyesha kabisa kwamba habari zimehamishwa tu kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Zamani wakati naripoti kwenye magazeti tulikuwa tunaelekezwa na wahariri wetu kuandika habari kutoka angle tofauti mara unapokutana na mwandishi mwenzio aliyetoka chombo unachokifanyia kazi ili msiandike habari inayofanana. Siku hizi mambo hayako hivyo, mtu mmoja anaweza kuandaa habari na kuzirusha kwenye blogs kubwa tano tofauti…NI AIBU!
Nawasihi mabloga wa bongo mjitahidi kuingia mtaani kutafuta habari na sio kukaa baa na kunakili tu habari zilizotolewa na wenzenu. Itaongeza msisimko zaidi pale utakapofungua blog ya Michuzi ukakuta ina picha ama habari tofauti na Mjengwa, au Michuzijr, au Mtaa kwa Mtaa, au Hakingowi. Na hata habari zikifanana, basi ziwe na taste tofauti. Ni dhahiri kwamba siku nyingine unakuta blogs zote zina kila kitu kinachofanana hata kama kuna typos.
Changamoto nyingine ninayopenda kuwagusia wanabloga hawa ni kuchangamkia breaking news. Kumekuwa na umaskini wa kuripoti matukio ya dharura au matukio mengine muhimu kutokana na kutohangaikia habari. Unaweza kukuta tukio lililotokea saa nane mchana linakuja kuripotiwa na magazeti kesho yake asubuhi, na hata bloga mmoja akilidaka hilo basi hiyo habari utaikuta kwenye blogs zote kwa staili ile ile ya mmoja! Na hii si sahihi kabisa maana hata sponsors wenu wanategemea kuona page zimesheheni habari na matukio yanayoendana na wakati. Hivyo nawasihi bloggers wetu mjishughulishe kupata habari.
Proofreading ama kuhakiki mnacho post ni ufa mwingine ambao si tu unakera bali pia unatia aibu kwa taaluma ya uandishi kwa ujumla. Imefikia mahali ambapo hata majina ya watu au vielelezo muhimu hukosewa bila hata mabloga hawa kusahihisha, ni jambo la aibu. Nisingetegemea kuona gazeti la mzalendo, nipashe, mwananchi nk zimetoa habari kwenye front page au kurasa nyinginezo na kukosea spelling halafu wakaendelea kwa mtindo huo bila kujirekebisha. Blogs zetu zinapaswa zifuate utaratibu wa kuzipitia na kusahihisha habari zao kabla ya kuzirusha.
Otherwise napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa kwenda na wakati, kwani bila kujitolea kwenu kuanzisha blogs tungekuwa tunapitwa na mambo mengi sana, lakini tunapaswa kupashana pale tunapoona panahitaji marekebisho ili twende sambamba na kasi ya dunia.
Mwandishi wa kujitegemea
6 comments:
NAOMBA NIANZE KWA KUSHUKURU NA KUTOA NENO MOJA TUU KWAMBA SIO KWAMBA TUNACOPY NA KUPASTE MDAU ILA HABARI UKIONA ZINAFANANA UJUE PIA BLOGGER HUYO KATUMIWA HIYO NUZ.. NA ANAESOMA BLOG YAKO SIE ATAESOMA BLOG YA MWENGINE KILA BLOG INA WATU WAKE ASANTE SANA
Very well done, nilifikiri ni mimi tu naboreka, most of hizi blog story na picha vina fanana. wanablog inabidi wabadilike kidogo. story zikiwa tofauti zinakua poa zaidi
Kaka Tino ungeandika jina tu...kama utaona picha zimefanana unaenda blog nyingine, unajua habari hizi huwa zinatumwa na watu so mtu mwenye blog anaweka kama alivyoombwa.
Tafadhali gonga link hapo chini itakuonyesha meli iliyozama august 2011 huko philipines MV malasia, chombo cha habari kimoja tu kilipoitumia picha hiyo, vyombo vya habari vyote vilikopi picha hiyo, hali ambayo imewafanya wanaichi wengi au wote kuona au kuamini hiyo ndio iliozama, meli ambayo abiria wake na macrew wote waliokolewa http://www.ibtimes.com/articles/191359/20110803/cargo-ship-sinks-in-seas-of-philippines-all-passengers-rescued-photos.htm
Karibu mwandishi
Karibu ujiunge nasi tuliowahi kuandika hapa vhttp://changamotoyetu.blogspot.com/2010/04/blog-zetu-na-maradhi-ya-bongo-flava.html
Mtoa hoja kama umeona habari ni hizo hizo basi tembelea nyingine. Angalia magazeti ya UK hasa habari za michezo, mara nyingi habari ni zile zile na magazeti yanauzwa tu. Au hata bongo, habari za magazeti ni zile zile...mimi naona nikutowatendea haki watu wenye blog hizi, wanafanya kazi kubwa na pia wanapokea habari hizi kwa watu na siyo kwamba wan copy na ku paste tu.
Post a Comment