ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 15, 2011

Jambo Africa Child Hope -Rambi rambi

SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA WALIOPATA AJALI YA MELI ZANZIBAR KUTOKA UONGOZI WA JAMBO AFRICA CHILD HOPE INC. ( USA).


Uongozi wa Jambo Africa Child Hope Inc.( USA) tumezipokea taarifa za kuzama kwa meli ya Spice Islander kwa hudhuni na masikitiko makubwa. Tulipata mshtuko mkubwa kwa vifo vya wananchi zaidi ya 200, ambao walikuwa wakisafiri katika chombo hicho.Haya ni maafa makubwa kwa nchi yetu, Watanzania kwa pamoja tupo na ndugu zetu kwenye kipindi hiki kigumu. Uongozi wa Jambo Africa Child Hope Inc. (USA),Tanzania nachukua fursa hii kutumia salamu za mkono wa pole wafiwa,walionusurika na kwa Watanzania wote kwa ujumla Ama kwa ndugu zetu walionusurika tunawapa mkono wa pole kwa misukosuko na majeraha makubwa waliyapata wakati wa ajali hiyo. Sisi ndugu zao tuliopo huku Amerika tunaungana nao katika kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yao na pia tunamuomba Mungu awafanyie wepesi wa kupona mapema ili kuweza tena kushiriki katika ujenzi wa Taifa letu.Pia tunapenda kuwashukuru viongozi wa serikali, mashirika ya serikali na sio ya kiserikali,pamoja na watu binafsi ,kwa juhudi kubwa walizozifanya za kuokoa maisha ya wananchi wezetu. Mwisho
Mwenyezi Mungu awape wafiwa wote subira na nguvu za kukabili msiba huu mkubwa wa Taifa letu na alaze roho za marehemu mahali pema peponi .
Amin.
Uongozi wa Jambo Africa Child Hope Inc. (USA)/Tanzania.
www.jamboafricachildhope.org

No comments: