ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 22, 2011

Kuliko kumruhusu ‘aruke ukuta’, bora penzi life

Kwanza nimshukuru Mungu kwa yale ambayo amekuwa akinitendea katika kila siku ya maisha yangu. Nimshukuru pia kwa kunipa uwezo wa kuandika yale ambayo yamekuwa yakiwasaidia watu wengi katika maisha yao ya kimapenzi.

Wiki hii nataka kuzungumzia jambo moja kwa uchungu mkubwa. Najua wapo watakaonishangaa kwa kuwa wenyewe wamekuwa wakilichukulia kuwa ni la kawaida ila wale wenye uelewa mkubwa wa mambo na wanaoyajali maisha yao, watanielewe na kukubaliana na mimi.



Tunapozungumzia masuala ya mapenzi, kuruka ukuta si neno geni lakini kwa kufafanua zaidi nazungumzia mapenzi kinyume na maumbile. Wataalam wa afya wanaeleza kuwa, kufanya  hivyo kuna madhara makubwa, nikipata fursa nitayazungumzia siku zinazokuja.

Hali ikoje?
Huko mtaani kuna watu ambao huwaambii kitu katika hili. Wameshalemaa kwa staili hiyo ya mapenzi huku wakichukulia poa, ili mradi maisha yao yanakwenda.

Ukiachilia mbali hao, wapo wanawake ambao wako kwenye ndoa, waume zao wanapowaomba penzi hilo wanashindwa kukataa.

 Wenyewe wanadhani kwamba, eti wakiwakatalia wataachwa kama siyo kutengeneza mianya ya kusalitiwa. Hilo si kwa walio kwenye ndoa tu, hata wale ambao wako kwenye uhusiano wa kawaida kuna wanaosumbuliwa na wapenzi wao katika hilo.

Anakudharau, hakuthamini
Naomba niseme kwamba, mume au mpenzi wako akikuomba penzi hilo ujue amekudharau sana. Yaani atakuwa hakujali, hakuthamini wala hakuheshimu.

 Anakuchukulia kama changudoa ambaye haoni hatari kufanya hivyo ili mradi fedha iwepo. Ifike wakati umuone yule anayekuomba penzi hilo kuwa ni muuaji asiyestahili kuendelea kuwa na wewe.

Hastahili kuwa na wewe kwa sababu, hafikirii madhara utakayoyapata baadaye, anachoangalia ni raha anayoipata yeye wakati huo.

Raha ni kwake tu
Mbaya zaidi inadaiwa kwa staili hiyo ya penzi mwanaume ndiye anayeweza kusikia raha tu lakini kwa wanawake wengi ni karaha, eti wanafanya tu ili kuwaridhisha waume/wapenzi wao, jamani hii ni akili au matope? Kwanza kwa nini uombwe penzi hilo? Yeye anakuchukuliaje? Mimi nadhani mpenzi wako akikuomba penzi hilo chukulia amekutusi.

jifunze kwa ushuhuda huu
Juzi nilikuwa nazungumza na mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mama Sabrina.

Maelezo yake yalinishangaza sana na wewe hebu msikilize, ujifunze kitu.

“Mume wangu alinioa mwaka jana, awali tulikuwa tunakwenda vizuri, nilikuwa najitahidi kumridhisha kwa njia halali na yeye alikuwa akidai nampa raha ambayo alikuwa akiitafuta kwa muda mrefu.
“Kilichonishangaza juzi usiku wakati tupo faragha, akaniuliza kama kweli nampenda, nilipomjibu ndiyo, akaniambia kama nampenda basi nimtimizie kile atakachoniambia. Nilishtuka lakini nikamjibu kuwa niko tayari.

 Akaniambia eti wanaume wenzake wanasema mapenzi kinyume na maumbile ni matamu sana.
“Sikuamini kile nilichokisikia, nilipomuuliza alikuwa anamaanisha nini, akarudia kuwa anataka nimuonjeshe penzi hilo. Kwa kweli nililia sana na kuanzia muda huo nikaanza kumchukia. Alivyoona nimekasirika, akanibembeleza na kuniomba msamaha.

“Nilimsamehe lakini sikuwa na hamu naye tena, nilimchukulia kuwa ni muuaji. Lakini kilichonishangaza ni kwamba, kuanzia siku hiyo akawa amebadilika sana.

Mapenzi yakapungua, akawa anachelewa kurudi nyumbani na akirudi hana taimu na mimi. Naumia lakini najua sababu ni mimi kumnyima penzi hilo haramu,” anasema mama huyo ambaye mwenyewe anadai, siku si nyingi ataomba talaka yake.

ukiachwa kwa kumnyima, poa tu
Wanaosalitiwa au kuachwa na wapenzi wao kwa sababu hiyo ni wengi huko mtaani, lakini nasema walioathirika ni wale wanaoijali miili yao.

Kama huyo mtu wako bila kumpa penzi hilo hatosheki, aende huko anakodhani atapewa, akuache wewe ukiwa salama. Usikubali kumfanyia mpenzi wako mambo ambayo ni hatari eti kwa kuwa tu unaogopa kuachwa, wakati mwingine kuwa na msimamo katika yale unayoamini kuwa hayafai.

 Ni hayo kwa leo, nakaribisha maoni na ushauri.


www.globalpubliishes.info

3 comments:

Anonymous said...

Hilo unalosema ni kweli na hakika, binafsi nilishamtahadharisha mapeeeeeeema shemej yenu, akae akijua kabisa kama anaugonjwa wa kuruka ukuta akaruke anakokujua, m hapana.
asante kwa msg nzuri, kiukweli huu mhezo umeshamiri sana siku hizi

Anonymous said...

Yaaa huu mchezo mchafu sana tena hata hizo kitchen party zinazoendelea,sijui makungwi,somo unakuta unao diriki kusema hiyo siyo haramu mie naomba utoe hayo madhara ili tujue nadhani ndiyo tutagopa

Anonymous said...

Tufafanulie jamani kuruka ukuta au kinyume na maumbile maana ni nini? Kiswahili chawa kigumu.