ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 14, 2011

MABALOZI WATIA SAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO,UBALOZI WA TANZANIA,WASHINGTON,DC

Mabalozi wanaowakilisha nchi zao kutoka nchi mbali mbali duniani kutoka Afrika,Ulaya,Asia,Marekani ya Kusini na Kaskazini na nchi za Ghuba  hapa Marekani,wamefika katika Ubalozi wa Tanzania(TANZANIA HOUSE) uliopo Washington,DC kujumuika katika kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia msiba mkubwa ulilikumba Taifa la Tanzania kufuatia kuzama kwa meli ya MV Spice Islander katika mkondo wa Nungwi ,Zanzibar. Mabalozi hao kwa wingi wakiongozwa na mabalozi  kutoka Zimbabwe,Bahrain,Nicaragua,Namibia,Spain,Swaziland,Fiji, Spain,Mexico,Oman, Russia na kadhalika walionyesha kuguswa na ajali hiyo na kwa pamoja waliwaombea wahanga wa ajali hiyo na kuwaomba  wafiwa pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na subira katika wakati huu huu mgumu kutokana na ajali hiyo mbaya katika historia ya usafiri wa majini visiwani Zanzibar.

No comments: