ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 22, 2011

Rais Kikwete akutana na viongozi mbalimbali wa dunia jijini New York

Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki- Moon kwenye Makao Makuu ya Umoja Mataifa jijini New York nchini Marekani.
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akihudhuria mkutano wa 'Social Good Summit' anapokea tuzo kutoka United Nations Foundartion for his work in Martenal Health and Social Media Commitment kutoka kwa Makamu wa Rais wa Public Policy of United Nations Foundation Mr. Peter Yeo katika sherehe fupi iliyofanyika jijini New York jana.
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye mkutano wa 'Social Good Summit' 
Rais Dr. Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Luxembourg, Mh. Jean Asselborn wakati wa kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York nchini Marekani jana.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akizungumza na Rais wa Slovenia Dr. Danilo Turk kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York jana. Viongozi hao wanahudhuria kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichoanza tarehe 19.9.2011.
Picha na John Lukuwi 

 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu wa Canada Mh Stephen Harper wakati viongozi hao walipokutana katika hoteli ya Intercontinental huko New York nchini Marekani. Viongozi hao wako nchini humo wakihudhuria mkutano wa 66 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ulioanza tarehe 19.9.2011. 
Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na viongozi mashuhuri duniani akiwemo Askofu Desmond Tutu kutoka Afrika Kusini (kushoto) na aliyekuwa Rais wa Finland Mheshimiwa Marti Artisaari (katikati) wakati wa special event on the implementation of the Global strategy for women's and children's health iliyofanyika katika hoteli ya Grand Hyatt katika jiji la New York nchini Marekani. Picha na John Lukuwi/mawasiliano Ikulu

No comments: