Friday, September 2, 2011

URBAN PULSE NDANI YA SPORAH SHOW!!

 Frank akijadiliana na Mish wakati wa kipindi cha chemsha Bongo
 Mish akikamua ndani ya Sporah show
 picha ya pamoja baada ya show
 Sporah akichana mistari kumjibu Mish
Urban pulse Ndani ya sporah show
Salam,
Kwa mara nyingine tena Frank toka Urban pulse na msaniii makini Fyah Sister wakiwa ndani katika studio za Televisheni zinazotengeneza kipindi mashuhuri cha Sporah Show.
 
Kipindi hiki  maarufu kiendeshwacho na Dada yetu Sporah hapa UK kinapatiakana katika Sky TV  chaneli 184. Frank na Fyah Sister walialikwa kwenye exclusive interview na Dada Sporah kuzungumzia hali ya promotion ya nyimbo na mixtape ya fyah sister iliyopo mtaani hivi sasa. Vilevile walizungumzia hali ya uhusiano wa ma promoter na wasanii pamoja  na mitihani gani wanakumbana nayo.
 
 Album ya Fyah Sister ambayo imetengenezwa katoka studio za urban pulse, ni moja ya albamu zinazokuja juu sasa hasa katika kundi la wasanii wa kike, kwani England kuna wasanii wachache sana wazuri wa kike. Pia kipindi kiliongelea hatua na mafanikio ambayo urban pulse wameyapata mpaka hivi sasa kwenye masuala ya mbalimbali. Unaweza kudownload au kusikiliza mixtape ya Mish inayoitwa Fire Brigade kupitia link hapo chini


Mish ni msanii mkali wa kike anaekuja juu hapa UK, amefanya maonyesho mengi ikiwepo Notting Hill Carnival, Derby, Centre Hall Westminister jijini london n.k. Pia amechaguliwa kuingia katika mchakato wa kumtafuta best MC katika shindano linaloitwa OPEN MIC litakalofanyika mwezi wa kumi na fainali zake kufanyika katika O2 Arena london.

Spora show imekuwepeo mstari wa mbele katika kusaidia, kuwahamisha  wafanyabiashara na wanaharakati wa Kiafrika hapa UK. Vilevile ni kipindi kinachopigania na kuangaza mapambano kuhusu maswala yanayowakabili jamii za kiafrika  uk, kama vile, domestic violence,child abuse,rape, teenage pregnancy na masuala mengine yanayoathiri jamii zetu.

Kipindi Hiki kitakuwa hewani mda sio mrefu kupitia Ben TV sky channel 184. Kwa maelezo zaidi tembelea Sporah Show Blog

Asanteni,

URBAN PULSE CREATIVE


No comments: