ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 20, 2011

HAPA NA PALE KATIKA PICHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Mama Graca Machel, wakati walipokutana katika viwanja vya Mozambique Heroes Square, wakati wa kumbukumbu ya kifo cha mwasisi wa nchi hiyo, Hayati Samora Machel, mjini Maputo jana. Kulia kwa Makamu ni Mama Zakhia Bilal na (katikati) ni Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Bi. Samia Hassan Suluhu (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Harry Kitilya kuhusu namna makontena yanavyochunguzwa na mashine maalum wakati alipotembelea Mamlaka ya Bandari Tanzania juzi. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Muungano, Bw. Baraka Baraka na Mukurugenzi Mipango Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Joan Mbuya.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya  Bw.Abbas Kandoro akiangalia moja ya vifaa  vilivyoko kwenye banda la Jiji la Mbeya  wakati alipopita kwa ajili ya kukagua mabanda ili kujionea mambo mbali mbali yanayooneshwa katika  uwanja wa Ruanda Nzovwe ikiwa ni maadhimisho ya  miaka 50 ya  uhuru.
Wanafunzi wa Chuo kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakiwa nje ya Benki ya NMB Makao Makuu, Barabara ya Maktaba wakilalamika kutoingiziwa pesa zao kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Mbunge wa Mufindi Kusini, Bw. Mendrad Ligola akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Seriakali (PAC) na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dar es Salaam jana. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mkoani Rukwa Bw. Ally Kessy Mohamed na Mbunge wa Musoma Mjini, Bw. Vicent  Nyerere.
Maofisa wa ubalozi wa Tanzania wanaofanya kazi katika balozi mbalimbali duniani wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (hayupo pichani) baada ya kufungua mafunzo ya kujengeana uwezo kwa maofisa wa ngazi za ubalozi, Dar es Salaam.(Picha kwa hisani ya Majira)

No comments: