ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 19, 2011

UN YAKARABATI MADARASA MAWILI SHULE YA MSINGI TANDALE KWA GHARAMA YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI TATU

 Baadhi ya wafanyakazi wa mashirika la Umoja baada ya kuwasili katika shule ya msingi Tandale iliyopo Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya  wiki ya maadhimisho  ya 66 ya  Umoja wa Mataifa ambapo mashirika hayo yamejitolea kukarabati madarasa mawili ya shule hiyo.
 Pichani Juu na Chini ni mafundi wakiendelea na kazi ya kukarabati sakafu za madara hayo.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akiwa na walimu wa Shule ya Msingi Tandale pamoja na wafanyakazi wenzake wa Umoja wa Mataifa wakipeana utaratibu wa kutekeleza kazi za kijamii shuleni hapo.
 
Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni Hassani Kalinga (wa pili kushoto) akimkaribisha Mwakilishi wa UNESCO na Mratibu Mkazi mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Vibeke Jensen (wa pili kulia). Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tandale Renatus Pallu na Kulia ni Diwani wa Kata ya Tandale Jumanne Mbunju.
 
Mwakilishi wa UNESCO na Mratibu Mkazi mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Vibeke Jensen akizungumza mbele ya Walimu na  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tandale ambapo shirika hilo limekarabati madarasa mawili ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa. Jensen amesema ni lengo la shirika hilo kuhakikisha Wanafunzi wanasoma katika Mazingira mazuri yatakayowawezesha kuwa na uelewa darasani. Katikati ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa UNIDO Bw. Emmanuel Kalenzi na Kulia ni Diwani wa Kata ya Tandale Jumanne Mbunju.
Afisa Habari wa UN Information Centre  Usia Nkhoma Ledama akitafsiri kwa lugha ya Kiswahili Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mwakilishi wa UNESCO na Mratibu Mkazi mwakilishi wa Umoja wa Mataifa  Bi.Vibeke Jensen.


 Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tandale.
 Baadhi ya wafanyakazi wa UN wakisililiza kwa makini hotuba ya Bi. Vibeke Jensen.
 Diwani wa Kata ya Tandale Jumanne Amiri  Mbunju akishukuru shirika hilo kwa kuichagua shule ya Msingi Tandale kwa kuifanyia ukarabati wa madarasa mawili ambapo pia ameliomba shirika hilo kuikumbuka shule hiyo tena mwakani  wakati wa maadhimisho kama hayo. Diwani Mbunju pia ametumia fursa hiyo kuwataka wazazi kushiriki katika kutoa michango ya kuboresha mazingira ya kata ya Tandale.
Kwa picha zaidi Bofya Read More.



  Ujumbe mahususi.
Baadhi ya Walimu wa Shule ya msingi Tandale.
 Pichani Juu na Chini  ni Mwakilishi wa UNESCO na Mratibu Mkazi mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Vibeke Jensen akionyesha mfano kwa vitendo wakati wa shughuli za ukarabati wa madarasa hayo.
 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa UNIDO Bw. Emmanuel Kalenzi akishiriki katika kusaidia kuzoa mchanga wakati wa kazi ya ukarabati wa madarasa mawili wa Shule ya Msingi Tandale uliodhaminiwa na Umoja wa Mataifa.
 Hapa ni kazi tu.
 Tunaweka Urembo pembeni tunapiga kazi: Hoyce Temu naye alishiriki.
 Umoja ni Nguvu: Wafanyakazi wa UN na Walimu wa Shule ya msingi Tandale wakionyesha Umoja wakati wa kazi hiyo.
 Usia Ledama naye hakubaki nyuma.
 Walimu nao walichapa kazi.
 Wafanyakazi wa UN wakiwa kazini
 Baadhi ya Wafanyakazi wa UN
 Wanafunzi wakifurahi na baadhi ya wafanyakazi wa UN
 Nakumbukia enzi zangu...... Hoyce Temu akipooza koo na  Ice Cream za Ubuyu shuleni hapo baada ya jua kali.
 Afisa Habari wa WFP Bi. Christine Massiaga akitoa neno la shukrani kwa niaba ya mgeni rasmi Mwakilishi wa UNESCO na Mratibu Mkazi mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Vibeke Jensen kwa walimu na wanafunzi wa shule ya Msingi Tandale ampapo amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii kwani wao ndio watakaokuwa wawakilishi wa Umoja wa Mataifa hapo baadae.
  Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Tandale Bi. Lucy Mwakibete akitoa shukrani za Shule kwa UN kwa niaba ya Mwalimu Mkuu Bw. Renatus Pallu ambapo ameshukuru Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa kukarabati sakafu za vyumba viwili vya madarasa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Milioni 3. Vilevile ametaja changamoto zinazoikabili shule hiyo ambapo amezitaja kuwa ni uchakavu wa Miundo mbinu, upungufu wa madawati, na ukosefu wa seti ya Kompyuta pamoja na mashine ya kudurufia.
 Mwalimu Lucy Mwakibete akikabidhi hotuba ya shukrani ya shule ya Tandale kwa Afisa Habari wa WFP Bi. Christine Masiaga.
Kwa herini watoto wazuri UN inawapenda na inawajali": Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akigana na wanafunzi wa shule ya Msingi Tandale.


No comments: