
LEO tunaendelea na sehemu ya pili ya mada tuliyoianza wiki iliyopita kuhusu tabia 10 hatari katika mapenzi. Twende pamoja...
Ni rahisi mwanaume kuvumilia kasoro chache alizonazo mwenzake, lakini siyo ya namna hii. Muhimu ni kutambua ya kwamba uvivu utakupunguzia heshima na mvuto wako katika mapenzi.
Aidha, kwa mwanamke ni janga ambalo mwanaume hatokawia kulikimbia. Unadhani atawezaje kuvumilia kuwa na mtu ambaye hajiwezi kwa lolote? Kujishughulisha hutaki, kuwajibika katika uwanja wa kuta nne ni ngoma nzito! Atajiuliza: Ni faida gani ya kuwa na wewe?
Ni rahisi mwanaume kuvumilia kasoro chache alizonazo mwenzake, lakini siyo ya namna hii. Muhimu ni kutambua ya kwamba uvivu utakupunguzia heshima na mvuto wako katika mapenzi.
Aidha, kwa mwanamke ni janga ambalo mwanaume hatokawia kulikimbia. Unadhani atawezaje kuvumilia kuwa na mtu ambaye hajiwezi kwa lolote? Kujishughulisha hutaki, kuwajibika katika uwanja wa kuta nne ni ngoma nzito! Atajiuliza: Ni faida gani ya kuwa na wewe?
UCHAFU
Tabia hii, inaenda sambamba na uvivu. Kwa kifupi ni kwamba uchafu ni matokeo ya uvivu. Mtu asiyejiweza kwa lolote hatomudu usafi, hivyo kutia sumu kwenye uhusiano wake.
Una tabia ya uvivu, kwahiyo ni mchafu, unapaswa kutambua kuwa mwenzi wako anakerwa mno na tabia yako. Anza kwa kujichunguza mwenyewe ili kujua wewe ni mchafu kwa kiwango gani. Jawabu lako, linaweza kukusaidia kwa kiasi cha kutosha, ikiwa utaamua kubadilika.
Unavaa nguo mpaka zinatoa harufu mbaya, ukiongea, unatoa hewa chafu ya mdomo, kuoga kwa wasiwasi hadi mwili unanata, unashindwa kudhibiti jasho lako, mpaka unawasumbua wenzako kwa sababu ya kikwapa, kwa hali hiyo unategemea nini?
Tuweke kituo kikubwa kwa leo, panapo majaliwa tukutane Jumatatu, tupate kuendelea na mada yetu hii. Ushirikiano wako bado nauhitaji, kwahiyo tumia namba yangu hapo juu kwa ushauri au maoni.
Kama utakumbuka vizuri shoga yangu, katika toleo lililopita la Ijumaa Wikienda, niliweza kuchambua sumu mbili kati ya 10 zinazounda mada hii. Sina shaka kwamba ulinisoma vya kutosha, hivyo nakuomba uungane nami tena leo ili tuendelee pale tulipoishia.
Nilieleza Uvivu na Uchafu kama sumu zinazoshabihiana, kwahiyo zimebaki nane. Kabla sijaendelea mbele, naona ni busara nikuulize swali moja; Umejifunza nini mpaka sasa, kutokana na mada hii? Jibu naomba unitumie kupitia namba ya simu iliyopo hapo juu.
UBISHI
Unyenyekevu ni mbolea ya mapenzi, kinyume chake ni sumu, ndiyo maana ubishi ukawa tindikali ya uhusiano. Changamoto hii, kama ingekuwa inaeleweka vizuri na kuzingatiwa inavyotakiwa, pengine kusingekuwa na watu wanaotengana.
Binadamu tumeumbwa na udhaifu, kwahiyo kukosea siyo vibaya kwakuwa ni sehemu ya maisha yetu. Pamoja na kulifahamu hilo, lakini wengi wetu huwa hatutaki kukubali ukweli katika yale tunayokuwa tumekosea.
Tunataka tushinde kwa hoja hata kwenye mambo ambayo tunastahili kuwaomba radhi wapenzi wetu. Kasumba ya namna hiyo huwaumiza wenzetu moyoni kwa sababu wao huamini wamekosewa, kwahiyo hutarajia angalau kuombwa msamaha.
Fikiria mpenzi wako amekufanyia kosa ambalo wewe unalitathmini kama ni kubwa, unamuweka chini unaongea naye, lakini mwenzako anakuruka futi hamsini. Hataki kukubali kosa na zaidi anataka mbishane mpaka majogoo yawike. Katika picha ya namna hiyo wewe utajisikiaje?
Maumivu utakayoyapata wewe, basi yaone kuwa ndiyo anayopata mwenzako kutokana na tabia yako ya kutotaka kukubali ukweli. Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, msemo huu una maana kubwa kwa sababu tunapenda kuwaona wengine wabishi, lakini yakiwa kwetu hatutaki kujikosoa.
KIBURI
Kama ilivyo uchafu unatokana na uvivu, ndivyo ilivyo kwa Ubishi unavyoleta Kiburi. Maana yake ni kwamba mtu unapokuwa mbishi kupitiliza, unavimba kichwa na huko ndiko kuelekea kwenye kiburi. Utaelezwa nini na wewe kila kitu unajua?
Asili ya mtu mwenye kiburi huwa na majivuno kwa kuamini kwamba hakuna kinachoweza kumbabaisha. Lakini mtu mwenye fikra hizi anakuwa amepigwa kikumbo na tafsiri ya mapenzi ambayo inasema ni mwiko kujifanya ‘much know’ mbele ya mwenzi wako.
Daima kila unaloelekezwa hufanyi, badala yake unakuwa mzuri katika kupuuzia mambo. Ukichekecha kichwa chako, utagundua kwamba upuuzi ni sehemu ya kiburi, mnapanga miadi wewe na sweetie wako mkutane mahali, lakini unaamua kutokwenda bila sababu ya msingi.
Mpo katika maongezi ya faragha, mwenzio anajaribu kukuelewesha katika maeneo ambayo huwa unakosea, lakini badala ya kupokea ukweli, unaamua kunyamaza kimya, halafu unamkunjia sura kana kwamba anachokwambia ni simulizi za kubuni. Hicho ni kiburi!
Ukweli upo hivi, mtu mwenye kiburi akiambiwa ukweli huamini ametukanwa, hivyo huzua visa vya uongo na ukweli ama kubisha bila hoja, ndiyo maana nilitangulia kusema kuwa kiburi ni zao la ubishi.
Kasumba hii ukiwa nayo ni rahisi kuachwa kwa sababu hakuna siku ambayo mpenzi wako atakuwa anajisikia faraja kuwa na wewe.
Itaendelea wiki ijayo.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment