
Binti wa Gaddafi aliyekuwa Luteni-Kanali
*Alikimbilia Algeria na mama yake
Ni mwanamke wa “hamu”. Mrefu kama baba yake, mwenye umbo zuri na sura yenye mvuto. Ni mwanasheria aliyewahi kuwa Balozi wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), Ukimwi na Haki za Wanawake Libya.
Alipewa wadhifa huo Julai 24, 2009. Hata hivyo, Februari, 2011 umoja huo ulimvua
wadhifa huo.*Alikimbilia Algeria na mama yake
Ni mwanamke wa “hamu”. Mrefu kama baba yake, mwenye umbo zuri na sura yenye mvuto. Ni mwanasheria aliyewahi kuwa Balozi wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), Ukimwi na Haki za Wanawake Libya.
Alipewa wadhifa huo Julai 24, 2009. Hata hivyo, Februari, 2011 umoja huo ulimvua
Pia – amini usiamini – alikuwa ni mwanajeshi mwenye cheo cha Luteni-Kanali! Ndivyo “zinavyokuwaga” familia za viongozi wa kijeshi ili kulidhibiti jeshi na kujua nyendo zake za siri.
Ni Aisha (au Ayesha) Gaddafi aliyezaliwa mwaka 1976, akiwa binti pekee wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi.
Alikuwa pia mjumbe muhimu wa Gaddafi kuhusu masuala ya nchi za nje.
Akipinga Marekani kuingilia vita nchini Libya, mwaka huu Aisha alipigwa marufuku kutoka nje ya nchi hiyo tangu Februari 26, kwa mujibu wa Azimio la 1970 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Mwaka huu alipoushitaki Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (NATO) kwa mashambulizi ya makazi ya Gaddafi yaliyomwua kaka yake, Saif al-Arab al-Gaddafi, mtoto wake (Aisha) mdogo wa kike aliyekuwa miongoni mwa wajukuu watatu wa Gaddafi waliouawa, umoja huo ulipuuza mashitaka yake.
Waasi walipoteka makazi yake Agosti 22, mwaka huu, miongoni mwa mali zake walizokuta ni kochi moja kubwa la dhahabu likiwa katika umbo la nguva na sura yake (Aisha) upande mmoja.
Pia palikutwa chupa kibao za pombe licha ya baba yake kuwapiga marufuku Walibya kutumia vileo.
Agosti 27, mwaka huu yeye, mama yake, na kaka zake Muhammad na Hannibal, walikimbilia Algeria na watu wengine ambao maofisa wa Algeria walisema walikuwa ni pamoja na watoto wengi.
Waliruhusiwa kuishi Algeria kwa sababu za kibinadamu, na kwa vile Aisha alikuwa mjamzito akikaribia kujifungua. Agosti 30, kweli alijifungua mtoto wa kike.
Aisha alikuwa mke wa kanali wa jeshi, Ahmed al-Gaddafi al-Qahsi, mpwa wa Gaddafi. Ahmed aliuawa Julai 26, mwaka huu wakati wa mapigano nchini humo.
Walipata watoto watatu na wa nne ndiye yule aliyezaliwa na Aisha huko Algeria.
Hata hivyo, Aisha alisema Septemba 2, mwaka huu kwamba baba halisi wa mtoto huyo ni Mmarekani, Raj Rajaratnam, jambo ambalo mwanaume huyo alilipinga akisema “hajawahi kumgusa mwanamke huyo kwa vile ni kichaa”.
Aisha amesema atamfungulia mashitaka Rajaratnam ili agharamie matunzo ya mtoto.
Pamoja na Algeria kuwapokea, baraza la mpito linalotawala Libya limekuwa likiitaka nchi hiyo iwarudishe watu hao Libya.
Ni Aisha Gaddafi, binti wa Muammar na Safia.
Chanzo GPL
No comments:
Post a Comment