WAKATI mataifa ya Magharibi yakilishinikiza Baraza la Mpito Libya ‘NTC’ kuanzisha uchunguzi wa kina kuhusu kilichosababisha kuuawa kwa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi wakati alikamatwa akiwa hai, kijana aliyejitapa kwamba ndiye aliyemfyatulia risasi, anasakwa.
Kijana huyo ambaye jina lake halijapatikana, yuko hatarini kuuawa na baadhi ya Walibya wanaoishi Mtaa wa Misrata, mjini Sirte nchini humo.
Wamesema kuwa, wakimkamata watamkata kichwa huku habari nyingine zikidai kuwa wanataka arejeshe pete ya ndoa aliyoivua kwenye kidole cha marehemu muda mfupi baada ya kifo chake.
Habari zinasema, watu hao walikerwa na vitendo vya kinyama alivyofanyiwa Gaddafi kabla ya kifo chake na kwamba hakuna usawa uliotendeka kama Taasisi za Haki za Binadamu zinavyotaka.
Inasemekana hadi sasa kijana huyo anayekadiriwa kuwa na miaka 32 amejificha sehemu isiyojulikana baada ya kubaini kwamba kulikuwa na makosa ya kiufundi wakati wa kuchukua video za kukamatwa kwa Gaddafi ambapo yeye hakutakiwa kuonekana sura.
Kufichwa kwa sura kwa watu wanaowakamata viongozi kulifanywa na Wamarekani wakati wa kumnasa aliyekuwa Kiongozi wa Irak, Saddam Hussein mwaka 2006.
Majigambo ya muuaji
Baada ya mauaji ya Gaddafi, video moja ilimuonesha kijana huyo akitamba mtaani kuwa yeye ndiye aliyefyatua risasi iliyomuua Gaddafi.

Kijana huyo alidai kuwa hakukubaliana na wazo la kumtia mbaroni kiongozi huyo akiwa hai na hivyo aliamua kumuua.
“Tulimkamata, nilimpiga usoni baadhi ya wanajeshi walitaka kumuondosha eneo lile na hapo ndipo nilipoamua kumpiga risasi mbili, moja kichwani nyingine kifuani,” alitamba kijana huyo.
Ili kuthibitisha madai yake, muuaji huyo alitoa shati alilolivaa Gaddafi siku hiyo likiwa limeloa damu, pia alionesha pete ya ndoa (ya dhahabu) aliyoichomoa kwenye kidole chake.
Msemaji wa NTC
Akizungumza na Channel ya Al-Arabiya, Msemaji wa NTC, Abdel Hafiz Ghoga alisema, watampeleka mbele ya sheria mtu atakayebainika kumuua Gaddafi kwa kumpiga risasi.

No comments:
Post a Comment