Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohamed Ali, alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
Mtuhumiwa wa wizi Bw. Saidi Dadi (18) mkazi wa Yombo kilakala, Manispaa ya Temeke aliyekamatwa akituhumiwa kuvamia Duka la dawa la Enol lililoko Mbande, Magengeni Dar es salaam na kuiba sh. 60,000 na kukimbia nzao, akiwa chini ya ulinzi wa polisi jana. (Picha na Mudhihir Mudhihir)
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi (kushoto) akikabidhi bendera ya taifa kwa timu ya taifa ya pool, ambayo imeondoka jana kwenda nchini Malawi kushiriki katika mashindano ya All Africa Cup, yanayotarajiwa kuanza Novemba 22 mwaka huu. (Picha na Victor Mkumbo)
Wanafunzi hawa ambao hawakufahamika madarasa na shule wanazosoma, walikutwa na kamera yetu wakigombea kunywa maji kwenye moja ya mabomba yaliyopo viwanja vya maonesho ya nane nane vilivyoko Msamala, Manispaa ya Songea jana.
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakisaidia kuliinua gari namba T 354 AGD Mitsubish Canter, lililogongwa na Daladala (halipo pichani) na kuanguka katikati ya Barabara ya Nyerere jana. Dereva wa gari hilo alijaeuhiwa vibaya.
Muuzaji wa ndizi mbivu Bi. Georgista Mniuka, akiandaa ndizi zake kwa ajili ya kuuza kijiji cha Litola, wilayani Namtumbo jana. Biashara hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa mitaji na maeneo rasmi ya biashara.
No comments:
Post a Comment