Dinna Maningo, Tarime
MAHABUSU anayeshikiliwa Gereza la Wilaya ya Tarime, mkoani Mara, amejitundika juu ya mti uliopo ndani ya gereza, lengo likiwa ni kushinikiza askari kumuua kwa kile alichodai amechoka na unyanyasaji.Ilikuwa jana majira ya saa moja asubuhi, mahabusu huyo alisikika akilia kwa sauti akiwa juu ya mti mrefu, huku akitamka maneno ya kutaka askari magereza wamuue.
Akiwa ameshikilia ameshika shuka na chupa ya soda mkononi, alikuwa akipasa sauti yake akituhumu askari magereza kwa kuwanyanyasa, ikiwamo kucharazwa viboko na kukosa chakula.
Hali hiyo ilisababisha wananchi kusogelea gereza kumsikiliza mahabusu huyo.
“Nasema leo nimechoka nataka askari mniue, tumechoka na unyanyasaji tunaofanyiwa humu ndani ya gereza, waandishi wa habari, watu wa haki za binadamu tusaidieni tunanyanyaswa,” alisika akipaza sauti juu ya mti na kuongeza:

“Leo sishuki chini nimejitoa kufa na askari yeyote atakayepanda juu ya mti nitajitupa chini, ikiwezekana nitajinyonga kwa shuka hili niueni.”
Mahabusu huyo aliendelea kutuhumu uongozi gereza hilo kuwa, kumekuwa na uhaba wa chakula huku wakilazimika kulala bila chakula, hali ambayo imesababisha baadhi yao kufikia hatua mbaya kutokana na njaa na wengine kufikishwa Hospitali ya Wilaya ya Tarime.
“Tunateseka nina siku mbili sijapata chakula, watu chakula ni kubahatisha. Jumatatu mahabusu mwenzetu alizidiwa kwa sababu ya njaa akapelekwa hospitalini bahati mbaya amekufa kwa uzembe, tunaugua lakini hakuna huduma hadi mtu azidiwe ndiyo apelekwe hospitali, heri nife kuliko kuendelea kuteseka,“ alilalamika mahabusu huyo.
Hata hivyo, uongozi wa gereza hilo ulipotakiwa kuzungumzia suala hilo, uligoma kwa madai kuwa siyo wasemaji.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele, alikiri kupata taarifa za tukio hilo lakini akakataa kulizungumzia kwa kile alichoeleza kuwa, wanaendelea na uchunguzi wa chanzo cha mahabusu huyo kuchukua hatua hiyo.
Pia, Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Dk Nega Marco, alikiri Jumatatu kupokea mahabusu aitwaye Stephano Eliud, akisumbuliwa na kuhara na kutapika.
“Tukamwongezea dripu mbili za maji, lakini ilipofika Novemba 15, saa 7:00 usiku alikufa, kwakweli tulimpatia huduma iliyokuwapo ingawa hospitali yetu hatuna maji, wagonjwa wanajinunulia dripu za maji wenyewe na sisi tunawatundikia, mgonjwa alifikishwa hospitali akiwa mzima na alikufa baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi, tumejitahidi kwa uwezo wetu imeshindikana,” alisema Dk Marco.

No comments:
Post a Comment