ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 14, 2011

Mario Monti Kiongozi mpya Italia-BBC

Waziri Mkuu Mario Monti


Mwanauchumi na Kamishina wa zamani wa Tume ya Ulaya, Mario Monti ametangazwa Kaimu Waziri Mkuu wa Italia kufuatia mazungumzo kati ya rais Giorgio Napolitano na wanasiasa wa Italia.
Baada ya kuitikia ombi hilo aliahidi kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuidhinisha mpango wa kubana matumizi ya serikali.Naye Waziri Mkuu aliyeachia madaraka, Silvio Berlusconi ametetea uwongozi wake katika hotuba kwa taifa.
Kama kiongozi aliye na wabunge wengi Berlusconi anatarajiwa kushinikiza uteuzi wa baadhi ya mawaziri wake kwenye serikali mpya.
Profesa Mario Monti kwa jina la utani 'Super Mario' ana umri wa miaka 68 na alisomea shahada ya Uchumi katika chuo cha Milan ambapo wawekezaji mashuhuri kutoka nchi ya Italia walipata masomo yao.
Baaadaye alisomea chuo cha Yale huko Marekani na kuwa mwanafunzi wa mshindi wa tuzo ya Nobel la Uchumi James Tobin.
Katika matamshi yake ya hivi majuzi ameelezea wazi azimio lake la kupeleka bungeni mpango wa kubana matumizi ambao serikali ya Berlusconi iliona vigumu kutekeleza.
Kati ya mpango huo ni pamoja na kupunguza mishahara ya wanasiasa . Wabunge nchini Italia hupata mishahara mikubwa iklinganishwa na wenzao barani ulaya.
Changamoto moja kwa Profesa Monti ni kuungwa mkono na vyama vingine vya kisiasa ili nchi hiyo iweze kutekeleza masharti iliyopewa na viongozi wa nchi za ulaya kama hatua ya kuzuia mdororo wa uchumi unaokumba kanda inayotumia sarafu ya Euro.
Kisiasa Profesa Monti hajulikani na bado atakabiliana ana upinzani kutoka Bwana Berlusconi ambaye bado ana ushawishi mkubwa na anaungwa mkono na idadi kubwa ya wabunge katika Senate.

No comments: