Friday, November 11, 2011

MJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA AWASILI NCHINI

Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama akimlaki Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho, alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, kwa ajili ya siku tatu hapa nchini kwa mwaliko wa CCM.
Juu na chini ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama akimtambulisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenerzi Nape Nnauye, alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, kwa ajili ya siku tatu hapa nchini kwa mwaliko wa CCM. Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha CCM, Mwigulu Nchemba. (Picha zote na Bashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake