ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 6, 2011

Dk. Shein akabidhiwa ripoti ya kuzama kwa MV. Spice Islanders



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, (pichani) amekabidhiwa ripoti ya kuzama kwa Meli ya MV. Spice Islanders na Tume ya Uchunguzi wa ajali hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Abdulhakim Ameir Issa.
 Dk. Shein alikabidhiwa ripoti hiyo jana katika Ikulu ya Zanzibar, ambapo alitoa pongezi kwa  tume hiyo kwa kazi kubwa iliyoifanya na hatimaye kuandaa ripoti inayoeleza juu ya tukio hilo.
  Alisema ripoti hiyo ni muhimu kutokana na tukio kubwa lililotokea la meli kuzama na kuua watu wengi na kuihakikishia tume hiyo kuwa ripoti hiyo itafanyiwa kazi.

 Aidha, Dk. Shein, aliahidi kuwa taarifa zaidi zitatolewa kwa wananchi juu ya uchunguzi huo, pamoja na hatua zitakazochukuliwa na serikali. 
Mapema Mwenyekiti wa tume hiyo ya uchunguzi wa kuzama kwa Meli ya MV Spice Islander, Jaji Abdulhakim Amer Issa, alimueleza Dk. Shein kuwa tume yake imeridhika na uchunguzi ilioufanya.
 Alitoa pongezi kwa ushirikiano mazuri iliyopata tume yake katika kipindi chote cha uchunguzi katika maeneo yote waliyopita, pamoja na watu na watendaji wote waliokutana nao. 
Dk. Shein aliunda Tume hiyo mwezi Septemba mara baada ya tukio la kuzama kwa meli ya MV Spice Islander ili  kujua ukweli kuhusu chanzo cha ajali hiyo.
CHANZO: NIPASHE

No comments: