Kuelekea msimu wa Sikukuu za Krismas na mwaka mpya, usafiri kwa abiria umekuwa mgumu, kama abiria hawa waliokutwa kituo Kikuu cha mabasi Msamvu, Mkoani Morogoro, wakisubiri usafiri wa kuelekea Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa chama cha Kijamii (CCK ) Bw. Costantine Akitanda, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu mapendekezo ya Kamati teule ya Bunge, iliyochunguza sakata la Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Renatus Moabhi.
Mwanafunzi huyu alikutwa na kamera yetu akiwa amejining'iniza kwenye Baiskeli ya mizigo inayotumia magurudumu matatu (Guta), wakati akitoka shuleni, kwenye Barabara ya Morogoro, Dar es Salaam jana.

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za
Nishati na Maji (EWURA), Bw. Titus Kaguo akitoa ufafanuzi wa kazi za EWURA kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati aliyevaa kaunda suti) na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Christopher Sayi walipotembelea banda la Mamlaka hiyo, Dar es Salaam Jana, wakati wa maonesho ya miaka 50 ya uhuru yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jana.(Picha kwa hisani ya Majira)

No comments:
Post a Comment