Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia), akisikiliza maelezo ya Mkaguzi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Abel Swai, jinsi madereva wazembe wanavyosababisha ajali, alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Ndani kwenye maonesho ya Wizara mbalimbali viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba, Dar es Salaam jana.
Waziri wa Katiba na Sheria Bi. Selina Kombani, akizungumza na wadau wanaopambana kukomesha ukatili wa kijinisia, wakati akizindua Kampeni ya Kuwa Mfano wa Kuigwa, Pata Heshima Bila Kutumia Mabavu, Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Bw. Abubakar Karsan (kushoto), akisaini hati ya makubaliano ya uratibu na ushirikiano kwa Klabu ya waandishi wa Mkoa Dar es Salaam (DCPC). jana, Kutoka kushoto ni Mwenyekiti Bi. Jane Mihanji, Rais, Bw. Keneth Simbaya na Makamu Mwenyekiti Bw. Benjamin Masese.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Bw. Sabasaba Moshingi (kushoto), na MKurugenzi wa Huduma za Kibenki wa CITI BANK Bw. Gasper Njuu, wakisaini mkataba utakaowezesha wateja wa benki hizo kupata huduma kwenye matawi ya benki hizo, Dar es Salaam jana.
Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), wakishangilia bao lililofungwa na Nurdini Bakari (wa kwanza kulia), katika mechi ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Tusker Chalenji, iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Kili Stars ilishinda bao 1-0.(Picha zote kwa hisani ya Majira)
No comments:
Post a Comment