ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 13, 2011

HAPA NA PALE KATIKA PICHA

Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara ya Nje (BET), Bw. Ramadhan Khalfan, wakati wa kufunga maonesho ya miaka 50 ya Uhuru, kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana, Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Bw. William Lukuvi.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Haruna Masebu, alipotembelea banda la Mamlaka hiyo,  Wizara ya Maji wakati wa maonesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam juzi.
Ofisa Ardhi, Maliasili na Mazingira wa Halmashauri ya Namtumbo Bw. Kiyungi Kiyungi, akitoa ufafanuzi kuhusu mpango wa wizara hiyo kuzuia ujenzi wa barabara ya kijiji cha Likuyuseko hadi Mto Mkuju, ambako kuna hazina kubwa ya madini ya Uranium.
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Bi. Awena
Said Sanani (kulia), akimkabidhi kadi mpya za Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Wananchi (CUF), mjumbe wa jumuia hiyo Bi. Fatma Fereji, wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Hoteli ya Bwawani, Zanzibar jana.
Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu Mkoa wa Rukwa,  Christopher Kopa (kushoto)akiambaa na mpira huku mlinzi wa Tanga, Basalile Mponjoli akitaka kumpokonya wakati wa mechi ya Kombe la Taifa, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Leaders, Dar es Salaam jana.Tanga ilishinda pointi 114-19
Rais  wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari ya Moroni,  nchini Comoro (STMMPM), Bw. Mohamed Abdou Soilihi,  akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, wakati akitoa tamko la kupinga Serikali ya nchi hiyo kuipa kampuni ya Ufaransa uendeshaji wa bandari bila kukubaliana na wafanyakazi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi, Bw. Musa Samizi (aliyesimama), akizungumza na msafara ulioshuka kutoka kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro (hawapo pichani) jana. wengine toka kushoto ni Mkurugenzi wa Zara Tours, Bi Zaynab Ansell, Meneja wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Tawi la Arusha, Bw. Willy Lyimo, Kulia Bw. Madaraka Nyerere.
Ofisa Miradi wa Kitaifa wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO), Bw. Victor Akim (kushoto), akimsikiliza Meneja Mkuu wa Mradi wa Mkonge, 'Energy Systems' (Mes), Bw. Gilead Kissaka, mwishoni mwa wiki, wakati akielezea jinsi mabaki ya mkonge yanavyotumiwa kuzalisha umeme katika eneo la Hale Mkoa wa Tanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro (ACP) Adolphina Chialo, akionesha magunia 12 yaliyojazwa bangi ndani ya gari ndogo aina ya Mark II namba T 602 ABJ juzi., wakati yakisafirishwa na anayedaiwa kuwa, askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Bulolo Milumbe.(picha kwa hisani ya Majira)

1 comment:

Anonymous said...

HUU NDIO UJINGA SANA TULIOLIMBIKIZWA NA WAKOLONI... OHH BANGI BANGI, SI NI MMEA JAMA? MBONA TUNASAHAU ALIYEUMBA? TULISHAKAA CHINI NA KUUCHAMBUA MBANGI? HEBU TUELIMIKE WAAFRIKA, MBONA WAJINGA HIVI...