Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini David Jairo
Waandishi wetu
UTATA mpya umegubika utekelezaji wa hatua za kuwachukulia hatua Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini David Jairo, Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kama lilivyoagiza Bunge hivi karibuni, baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ‘kurushiana mpira’ na mawaziri wake juu ya nani anayestahili kutekeleza maagizo ya Bunge.
Bunge katika mkutano wake wa tano liliagiza Serikali iwachukulie hatua za kinidhamu Jairo na Luhanjo, huku Utouh akitakiwa kuchukuliwa hatua kwa kushindwa kufanya kazi yake vizuri.
Wakati Jairo akidaiwa kuchangisha fedha kwenye taasisi zilizoko chini ya wizara yake ili kupitisha bajeti ya wizara hiyo kinyume na sheria, Utouh na Luhanjo wanadaiwa kuboronga kazi kwa kutoa taarifa iliyomsafisha Jairo na Ngeleja kutokana na kushindwa kuwajibika kama msimamizi wa wizara.
Hivi karibuni kwa nyakati tofauti, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe, walikaririwa na vyombo vya habari wakieleza kuwa suala la vigogo hao lipo kwa Waziri Mkuu ambaye ndiye anapaswa kulitolewa maamuzi.
Lakini juzi Ofisi ya Waziri Mkuu, iliwataka mawaziri hao kuacha kukwepa wajibu na majukumu yao katika kutekeleza maagizo hayo ya Bunge.
Katibu na Msaidizi Maalumu wa Waziri Mkuu Pinda, Celestine Mushi, aliliambia gazeti hili kwamba, kauli ya Waziri Chikawe kuwa suala na jalada la maamuzi kuhusu hatima ya vigogo hao liko kwa Pinda, ni kujaribu kukwepa jukumu na wajibu wake wa kushughulikia jambo lililo ndani ya uwezo na mamlaka yake.
"Mimi nimepitia barua na majalada yote ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kabla sijaondoka ofisini Dar es Salaam. Hakuna barua wala faili linalohusu suala la azimio la Bunge kuhusu jambo hilo," alisema Mushi akiwa ziarani na Waziri Pinda mjini Moshi.
Akifafanua, Katibu huyo alisema mamlaka ya nidhamu ya makatibu wakuu wa wizara ikiwamo ya vigogo hao, iko chini ya Ofisi ya Rais na Chikawe ndiye Waziri wa Utawala Bora, hivyo ni jukumu na wajibu wake kulishughulikia
au kulizungumzia badala ya kuirushia mpira Ofisi ya Waziri Mkuu.
"Chini ya Ofisi ya Rais ndiko iliko Wizara ya Utumishi na Utawala Bora. Washughulikie hilo. Waziri Mkuu anatokea wapi kwenye suala la Jairo kuwajibishwa? Viongozi wasikwepe majukumu yao!" Alisisitiza Mushi.
Awali, Mushi aliyekuwa katika msafara wa Pinda kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Taasisi ya Maendeleo Kilimanjaro (KDF), aligoma kuwaruhusu waandishi wa habari wa gazeti hili kufanya mahojiano ya ana kwa ana na Waziri Mkuu, baada ya kuelezwa kwa nini wanataka kumuona.
"Katika hili sitawapa fursa ya kuonana na PM (Waziri Mkuu). Jamani msimuonee bosi wangu kwa sababu ni mpole. Hapa atazungumzia masuala ya KDF basi. Nje ya hapo hapana na iwapo kuna haja ya yeye kuzungumzia suala la Jairo, nitamwandalia forum (jukwaa) nzuri Dar es Salaam, akutane na wahariri azungumze nao," alisema Mushi.
Hata hivyo, baada ya kuelimishwa kwamba Pinda ndiye anayepaswa kujua suala hilo kwa kuwa mawaziri wenzake wamesema wameshampatia kwa hatua zaidi, Mushi alijibu: "Mawaziri hawa waache kukwepa majukumu na wajibu wao katika mambo yaliyo chini au ndani ya uwezo wao."
Majibu ya Ghasia
Hivi karibuni Waziri Ghasia aliwaambia waandishi wa habari kuwa, “Suala la vigogo hao akiwamo Jairo, lipo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.”

Hata hivyo, alipotakiwa tena juzi kuzungumzia majibu hayo ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ghasia alisema "suala hilo halipelekwi kwa Waziri Mkuu na ofisi yangu, bali Bunge."
Aliongeza, “lakini kuna mambo mengine mengi ya kuandika, siyo lazima mkang’ang’ania hilo moja la Jairo na mimi siwezi kusema mengi kwa sasa sipo ofisini, nipo Ufaransa.”
Ofisi ya Bunge
Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashililah alipotakiwa kuzungumzia suala hilo jana alisema; "Sielewi kama lilishapelekwa kwa Waziri Mkuu au la."
Kashililah aliongeza; “Sina hakika kama hiyo ripoti imepelekwa ama la. Lakini mtafute Joel (Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge, John Joel) atakuelezeni.”
Kauli hiyo ya Dk Kashililah inapingana na aliyoitoa Desemba 7 mwaka huu aliposema ripoti hiyo imeshawasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu."Ni kweli Ofisi ya Bunge imewasilisha taarifa ya Azimio la Bunge serikalini, kwa kawaida sisi tunawasilisha taarifa kama hiyo Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye ndiye Mkuu wa Shughuli za Serikali ndani ya Bunge," alisema Dk Kashililla na kuongeza:
“Kwa kawaida tunachukua saa 72 tu kuwalisilisha Azimio la Bunge serikalini baada ya Bunge kuahirishwa, sisi kama Bunge tumemaliza kazi yetu labda tusubiri tu maamuzi ya serikali."
Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge, Joel alisema taarifa za suala la Jairo zilishatoka katika Idara yake.
“Kwa wangu, hiyo taarifa imeshatoka katika Idara yangu, itakuwa imeshapelekwa kwa waziri husika,” alisema Joel.
Alipoulizwa kwamba suala hilo limepelekwa kwa Waziri gani, alisema hawezi kujua kwa sababu barua za kupeleka taarifa hizo, zinaandikwa na Katibu wa Bunge.
“Ninachofahamu ni kuwa zimepelekwa kwa mawaziri husika, ila siwezi kukumbuka ni waziri yupi haswa kapelekewa kwa sababu anayeandika barua ni Katibu wa Bunge mwenyewe,” alisema Joel.
Akiwasilisha taarifa ya uchunguzi wa suala hilo, Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Injinia Ramo Makani (CCM) alisema kutokana na utaratibu huo, ni vyema Bunge likaendelea kukemea kwa nguvu zote utaratibu wa uchangishaji wa fedha uliofanywa na wizara hiyo.
"Kamati teule inapendekeza kwamba serikali ichukue hatua za kinidhamu kwa ndugu David Kitundu Jairo, kwa matumizi mabaya ya madaraka, kukusanya na kutumia fedha za serikali kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za umma na kuruhusu matumizi mabaya ya fedha za umma," alisema.
Mbali na hatua hizo kwa Jairo, pia kamati hiyo imependekeza watumishi wote wa wizara hiyo ambao waliainishwa katika taarifa hiyo wachukuliwe hatua za kisheria.
"Aidha, kwa kuwa waziri kwa mujibu wa mwongozo wa Baraza la Mawaziri ndiye msimamizi mkuu wa wizara, hivyo suala la uchangishaji halikupaswa kufanyika bila yeye kufahamu, Kamati teule inapendekeza serikali ichukue hatua zinazofaa kwa Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa William Ngeleja ambaye ni mbunge," alisema Makani.
Alisema kamati yake ilisikitishwa na jinsi CAG, Utouh alivyoshindwa kutekeleza wajibu wake kikamilifu.
"Hususan katika kulisaidia Bunge na umma kwa ujumla, Kamati teule inapendekeza serikali ichukue hatua zinazofaa kwa CAG kwa upotoshaji huo," alisema Makani.Katika hatua nyingine, kamati hiyo ilipendekeza Katibu Mkuu Kiongozi, Luhanjo achukuliwe hatua zinazofaa na Serikali.

Imeandikwa na Fredy Azzah Dar, Peter Saramba na Rehema Matowo, Moshi wa Mwananchi.
No comments:
Post a Comment