ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 23, 2011

Kituo cha kusaidia waathirika wa mafuriko chafungwa-Mwananchi

Keneth Goliama
KITUO cha kupokelea watu walioathirika na mafuriko katika Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam kimefungwa baada ya  wathirika wa maafa ya Mvua kutojitokeza.Kituo  hicho ambacho kipo Shule ya  Kibasila, Wilaya ya  Temeke, mkoani Dar es Salaam baada ya waathirika kutokwenda katika kituo hicho tangu jana.

Kwa mujibu wa Mlinzi wa Shule ya Kibasila Mandina Buku, alisema tangu kituo hicho kiandaliwe kwa ajili ya kupokea waathirika wa mafuriko, hakuna hata mtu mmoja aliyefika pale kupata huduma.
Alisema wasimamizi wasaidizi wa  maafa, walikaa muda mrefu, lakini watu hao hawakufika kupata msaada.

Katika hatua nyingine, Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Temeke, Shamimu Ronda alisema mtu mmoja tu, alifika katika hospitali hiyo baada ya  kuangukiwa na ukuta katika maeneo ya Mbagala.

Ronda alisema hakuna majeruhi  zaidi waliofikia  katika hospitali ya Temeke tangu jana baada ya kutokea mafuriko makubwa jijini Dar es Salaam kuanzia juzi.

Uwanja wa  wa Ndege
Uwanja wa Ndege wa Mwlimu Julius Nyerere ulionekana kuendelea kutoa huduma ya usafiri licha ya maji kujaa katika uwanja huo.Mwananchi ilifika katika uwanja huo na kuona  wasafiri wakiendelea na shughuli zao kama kawaida na wengine ndai ya uwanja na kutoka.

No comments: