ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 23, 2011

Kulipa kisasi katika mapenzi ni kutengeneza kosa - 4

NAAM tupo pamoja kama kawaida yetu mu hali gani popote mlipo wapenzi wa kona yetu ya mahaba.
Tuendelee na kiporo chetu ambacho kinafikia tamati wiki hii. Tunaangalia jinsi mtu anavyoweza kupenda kupitia macho, anachokiona na kinachomvutia ni umbile lakini kitu muhimu kuliko vyote ni tabia ya mtu hapo ndipo nilipo sema bahati nasibu.
Huwezi kuijua tabia ya mtu kwa kupima kwa macho zaidi ya kuvutiwa na umbile na sura tu. Hapa wengi ndiyo hucheza bahati nasibu. Wapo wanaowachunguza watu kabla ya kuwa nao na kuridhika na tabia zao, lakini labda tabia uliyoiona ni ya kutengeneza, ikitokea ukawa naye ndipo huitoa tabia ya asili.

Hapa wenye tabia za chui huzificha kwenye ngozi ya mbuzi ili kutafuta kitu fulani na wakipatacho hurudia tabia zao.
Mtu kama huyu huwezi kumlaumu, mara nyingi unapompenda mtu aliyekukubali kwa sababu fulani huwa hana mapenzi ya kweli.
Hebu tuangalie kitu kimoja muhimu katika uchaguzi wa mpenzi ambaye nina imani ndiye atakaye kuwa mkeo au mumeo ambaye hatachosha machoni na akili.
Naimani kila mmoja ana vitu ambavyo humvutia kwa mtu, sehemu hii humpendelea sana mwanaume ambaye mara nyingi ndiye mchaguzi.
Hii sehemu muhimu naomba uelewe usije sema eti ulikurupuka au uliweka matamanio ya mwili mbele.
Hakikisha uchaguzi wa kwako wa kwanza unakuwa wa makini ambao hautaujutia maishani mwako na kuona kama mpenzio umempata usiku wa kiza na kushindwa kufikisha kile ulichokitaka katika maisha yako.
Upo na mwenza wako ndani lakini bado mtu akipita unachanganyikiwa na kuona kama mpenzio ulipewa kama nyongeza, la hasha. Ni makosa makubwa kufanya majaribio katika mapenzi, pia ni kosa kubwa kumvulia nguo mtu usiye mpenda, upe hadhi mwili wako uonekane kwa yule uliyemchagua kwa moyo wako siyo kwa macho kwa sababu macho kuona ni kazi yake.
Fanya uchaguzi kwa kile ambacho umekifanyia uchunguzi kwa muda mrefu kuchagua mpenzi kwa kurupuka ni makosa, weka subira kwa kumtafuta ambaye hutasita kumtambulisha mbele za watu kuwa mke au muwe wangu au rafiki yangu wa kiume au wa kike.
Ni makosa kujiingiza kichwakichwa kwenye mapenzi bila kujua kina chake, utakufa maji, mapenzi ni kama maji yaliyo tulia lakini kina chake ni kirefu sana kinaweza kukumeza na kukupoteza katika dunia hii.
Usimpende asiyekupenda ukilazimisha penzi ndiyo mwanzo wa kufanyiwa mambo kwa kisingizio eti umemsingizia anatembea na fulani.
Namalizia kwa kusema hivi, penye penzi la kweli hakuna hujuma wala kisasi pasipo na hujuma hakuna kisasi, penye kisasi hakuna mapenzi funguka macho

Tuonane wiki
ijayo kwa
mada mpya.

www.globalpublishers.info

1 comment:

Anonymous said...

Leo umeongea kitu cha maana. Ni kwelikabisa hayo uliyoyasema.