ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 16, 2011

Misa Kwa Kiswahili Sahihisho Misa ni Januari-8-2012

Ndugu Watanzania na wote wapendao Misa Takatifu wa Lugha ya Kiswahili.

Karibuni tuendeleze tulichokianzisha:-

Misa Takatifu Itafanyika Tarehe 8 Januari 2012 Saa 8:00 Mchana. Liwe liwalo tujitahidi kushiriki.

Mahali:-  St. Edward R.C. Church,
                901 Poplar Grove St.
                 Baltimore, MD 21216

Baada ya Misa tutakuwa na viburudisho katika Ukumbi wa Parokia   2848 W. Lafayette Avenue, Baltimore, MD 21216.

Karibuni wote. Tafadhali Mjulishe yeyote unayejua anapenda kujiunga nasi. 

Weka Alama kwenye Kalenda yako:-
1. Misa nyingine itakuwa Pasaka - Aprili 8, 2012 
2. Itakayofuata itakuwa  - Julai 1, 2012
3. Nyingine itakuwa  - Septemba (tarehe bado)
4. Itakayofuata itakuwa  - Novemba 4, 2012 Nia ni uwakumbuka Marehemu wetu
5. Ya kufunga mwaka huo itakuwa  Decemba 9 Kuadhimisha Uhuru wa Taifa letu.

Tunatumaini tutaweza kuwapa taarifa kamili ni wapi misa zitafanyika mapema iwezekanavyo.
Karibu - Karibuni sana. Heri kwa Noeli na Baraka tele kwa Mwaka Mpya.

Padri Shao

No comments: