
MIMI mzima jamani na acha niende moja kwa moja kwenye mada niliyoianza wiki iliyopita.
Kimsingi wapo wanaoweza kukabiliana vilivyo na tamaa zao, hawa ni wale wanaowaheshimu wapenzi wao, wanaoweza kutafuta njia mbadala za kuziridhisha nafsi zao pale hisia za kufanya mapenzi zinapowajia.
Kimsingi wapo wanaoweza kukabiliana vilivyo na tamaa zao, hawa ni wale wanaowaheshimu wapenzi wao, wanaoweza kutafuta njia mbadala za kuziridhisha nafsi zao pale hisia za kufanya mapenzi zinapowajia.
Kwa maana hiyo si suala gumu sana kujizuia kumsaliti mpenzi wako hata kama yuko mbali na wewe. Unachotakiwa kufanya ni kutengeneza mazingira ambayo hayatakufanya ‘ummisi’ sana.
Ni mazingira yapi?
Unapokuwa mbali na mpenzi wako kuna njia mbalimbali zinazoweza kukufanya ukawa karibu naye na kila mmoja akazishinda tamaa zinazoweza kumfanya amsaliti mwenzake.
Ifahamike kwamba, ukiwa mbali na mpenzi wako suala la gharama ili kutengeneza mazingira ya ukaribu si jambo la kuepukika. Hivyo kuwa tayari kutumia gharama yoyote kumfanya mpenzi wako asikumisi kwa kufanya yafuatayo:
Mawasiliano yasiwe haba
Hii ni moja ya njia ya kumuweka karibu mpenzi wako hata kama yuko mbali na wewe. Hakikisha haipiti siku bila kuwasiliana naye na ikipita jione kwamba umefanya kosa kubwa sana.
Hata kama uko bize sana, hakikisha unatenga muda mfupi wa kumpigia simu au kumtumia sms. Kanuni rahisi ya mawasiliano kwa mpenzi wako iko hivi; asubuhi muamshe kwa ujumbe mzuri wa simu au ikiwezekana mpigie kabisa simu ukimtakia asubuhi njema kisha baada ya hapo, weka pozi.
Mchana fanya hivyo kwa kumtakia mchana mwema na jioni mtumie sms ya kumpa pole kwa mihangaiko ya siku nzima. Usiku ndiyo inakuwa funga kazi. Wakati huu tumia muda mwingi kuongea au kuchati naye tena wote mkiwa kitandani. Pozaneni kiu kwa kufanyiana utundu wa kimahaba wa hapa na pale.
Kama huujui utundu huu ambao unaweza kumfanya mpenzi wako akamaliza hata ile hamu ya kufanya mapenzi, nipigie nitakusaidia. Baada ya hapo, takianeni usiku mwema.
Kwa mawasiliano hayo naamini utakuwa umemuweka karibu zaidi mpenzi wako na utakuwa umemuondoa katika mazingira ya kukusaliti. Akikusaliti huyo hana mapenzi ya dhati na wewe na huenda ni mtu anayeweza kukusaliti hata kama hamko mbali.
Funga safari
Usikubali kuwa mbali na mpenzi wako kwa muda mrefu bila kuonana naye. Kama yuko nje ya nchi hiyo ni ishu nyingine lakini kama wote mko Tanzania, panga utaratibu wa kwenda kumtembelea hasa pale mnapoona mmekumbukana sana.
Kwa nini?
Jamani sisi wote ni watu wazima, unapokuwa na mpenzi kuna wakati unajisikia hamu ya kuwa naye faragha. Hilo lipo kwa wengi na baadhi wanapojiwa na hamu hiyo hulazimika kuwapigia simu wapenzi wao na wakiulizwa sababu ya kupiga simu utasikia; ‘Nimekukumbuka na nimetamani tu kusikia sauti yako’.
Hata hivyo, hamu hii inavumilika na mtu anaweza asimsaliti mpenzi wake lakini muda wa kuwa mbali ukizidi, kunakuwepo mazingira mazuri ya watu kusalitiana.
Hivyo basi, panga angalau hata kwa mwezi mara moja kama hamko mbali sana au kama ikishindikana basi iwe hivyo mara moja kwa miezi mitatu. Hiyo itakupunguza kasi ya kusalitiana.
Ni hayo tu kwa leo, tukutane tena wiki ijayo.
www.globalpublishers.info.
No comments:
Post a Comment