
MJADALA ni mkubwa sana juu ya mada hii.
Wengi imewagusa, lakini kuna makundi mawili; wapo waathirika ambao wanatamani kuachana na utumwa huu na wengine wameathirika zaidi, kiasi kwamba hawana mpango wa kuacha.
Wengine wameenda mbali zaidi, kwa vile
hawafikirii kuachana na mchezo huu, wamefikia hatua wanasema kwamba hakuna madhara kwa mtu anayejichua! Nimepokea simu nyingi sana, meseji nyingi na wengine wamejadiliana pamoja na marafiki wengine kwenye ukurasa wangu wa facebook.Wengine wameenda mbali zaidi, kwa vile
Katika mtandao wetu wa globalpublisherstz.com, mjadala ulikuwa mkubwa zaidi.
Watu wanatetea wazi wazi, kwamba kujichua hakuna madhara. Sikia rafiki yangu, hata anayevuta sigara anajua kwamba ina madhara kwa afya yake, lakini ili kujifariji, atajenga hoja kwamba, haimdhuru na badala yake inamsaidia sana kuondoa baridi na haina kilevi.
Wakati mvuta sigara akisema hivyo, mlevi naye atakuja na hoja kwamba, pombe inamsaidia sana kupunguza mawazo. Kila mmoja atatetea upande wake. Ni jambo la kawaida kabisa.
Nikiwa naelekea kuendelea na mada yetu, rafiki yangu mpendwa kama wewe ni ‘muumini’ wa tabia hiyo, unatakiwa kufahamu kwamba unafanya jambo HATARI sana, si tu kwa afya yako, kisaikolojia na dhambi ya uzinifu ambayo hiyo itatokana na uhusiano wako mwema na imani ya dini yako, NDOA yako ipo/itakuwa hatarini.
Nadhani mnakumbuka wiki iliyopita nilieleza maana ya kujichua, namna tendo linavyofanyika na jinsi mtu anavyoanza mchezo huo bila kutegemea. Sasa rafiki, hebu tuendelee kwenye namna tatizo linavyokua.
UKUAJI WA TATIZO
Mwathirika akishazoea, hufanya tendo hilo kama sehemu ya maisha yake. Alianza bila kujua matokeo yake, lakini sasa amejikuta akianza kuupenda na idadi ya ufanywaji wa tendo huanza kupanda, baada ya siku tatu, siku mbili, kila siku na hatimaye kwa siku zaidi ya mara moja.
“Kaka Shaluwa, najichukia sana, yaani nimekuwa mtumwa kabisa wa kufanya huu ujinga.
Kwa siku nafanya mara mbili au zaidi, lakini si chini ya hapo,” alisema rafiki mmoja, aliyenipigia simu baada ya kusoma sehemu ya kwanza ya mada hii wiki iliyopita.
Ukweli ni kwamba, mfanyaji kwa vile ameshapata ‘mteremko’ wa kutimiza haja zake, kwanza ataanza kuwadharau wanawake/wanaume, kwamba hawawezi kumtisha, kwa sababu ana njia za kujifurahisha mwenyewe.
Pili, hufikia hatua ya kuwachukia watu wa jinsia pacha, akiwaona kama ‘wanaringa’ hasa kama atakuwa amemshawishi kimapenzi na kukatawaliwa.
ATHARI ZAKE
Zipo athari nyingi sana ambazo mwathirika anaweza kuzipata kwa kuendekeza mchezo huu. Hapa nataka nizungumze kwa herufi kubwa kabisa kwamba, ndugu zangu usidanganyike kwamba hakuna madhara kwa kufanya mchezo huu.
Yapo MADHARA makubwa sana ambayo yanapatikana kwa mchezo huo. Achana na propaganda za mitaani, zenye utafiti hewa.
Sikia nikuambie rafiki yangu, hasa wewe ambaye unafanya mchezo huo. Upo kwenye hatari kubwa ya kushindwa kufurahia mapenzi, kwa vile mazoea ya kiungo siri chako ni kwenye vitu ‘artificial’ zaidi ya ‘natural’.
Mwanaume aliyezoea kujiridhisha mwenyewe, akikutana na mwanamke, hana muda mrefu sana, kila kitu kinamalizika.
Siyo hivyo tu, uwezo wa kurudia tendo unakuwa mdogo au unakosekana kabisa. Kinachotokea ni kwamba, kiungo siri chake kinakuwa kimeshazoea, aina nyingine ya ‘hali ya hewa’ hivyo kinapokutana na sehemu siri za kike, ambazo ni laini na zenye ute mwepesi, inakuwa rahisi kumaliza ‘biashara’ mapema wakati wateja bado wanahitaji!
Kiungo siri cha mwanaume huwa kigumu, hivyo kusababisha maumivu kwa mwanamke kutokana na sugu aliyoitengeneza bila kujua. Kwa kawaida viungo siri vyote ni laini sana na vinatakiwa kubaki katika hali hiyo ili kuleta msisimko wenye usawa.
Mazoea yoyote tofauti na yale ambayo yanatakiwa hupunguza msisiko na kusababisha mmoja wa washiriki wa tendo la ndoa kubaki na kiu na mwenzake.
“Najuta kuufahamu huu mchezo, kila siku ninapokutana na mume wangu, ananiacha nikiwa sijatosheka. Kiukweli tangu amenioa, sijawahi kufurahia tendo la ndoa. Nilianza huu mchezo zamani sana, tangu nikiwa kidato cha tano.
“Kuna rafiki yangu mmoja nilikuwa nakaa naye bweni moja alinifundisha. Sikujua kama madhara yake ni makubwa kiasi hiki. Ilikuwa ni shule ya wasichana tupu, kwa hiyo akanidanganya kwamba tuachane na wanaume tujichue...kumbe alikuwa ananisaga!” hii ni sehemu ya ushuhuda mwingine wa mchezo huo.
Athari nyingi ambayo mtu anaweza kuipata kwa kujichua ni kumaliza ‘kazi’ mwenyewe bila hata kwenda kazini. Akipita mtu wa jinsi pacha, ambaye ana mvuto, kazi inaishia hapo hapo!
UPO KUNDI GANI?
Uko wapi rafiki yangu? Nazungumza na wewe ambaye unafanya mchezo huo, bado unataka kuendelea nao au unatamani kuacha? Shika maneno yangu, kwamba ni HATARI kujichua, halafu weka nia ya kutaka kuacha huu utumwa, kisha vuta subira hadi wiki ijayo katika sehemu ya mwisho ambayo haitaacha kitu.
Ningeweza kumaliza mada leo, lakini nafasi ni ndogo rafiki yangu.
Ahsante sana kwa kunisoma, wiki ijayo ni muhimu sana kwako, USIKOSE!
Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers, ameandika vitabu vya True Love na Lets Talk About Love vilivyopo mitaani.
No comments:
Post a Comment