![]() |
| Rais wa Zanzibar DK Ali Mohamed Shein |
Ripoti hiyo ilikabidhiwa mwanzoni mwa mwezi huu kwa Rais wa Zanzibar DK Ali Mohamed Shein na Mwenyekiti wa Tume ya uchunguzi wa ajali hiyo Jaji Abdulhakim Ameir Issa.
Tume hiyo iliteuliwa baada ya meli hiyo kuzama katika eneo la Nungwi Septemba 10, mwaka huu na kusababisha watu 203 kupoteza maisha, 619 kuokolewa na wengine 1,764 mpaka leo hawajaonekana.
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kombo Dadi Maalim, alisema inashangaza wiki tatu baada kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi serikali imeshindwa kuiweka adharani kama ilivyoahidi kuwa matokeo ya uchunguzi yatakuwa ya uwazi.
“Serikali iliaahidi kugawa ubani kwa wathirika wa ajali hiyo, lakini mpaka sasa mwezi wa nne hakuna kinachoendelea,”alisema Kombo.
Alisema ubani huo kwa njia ya misaada ya fedha ungesaidia familia za wathirika, nyingine ambazo zimepoteza ndugu zao.
Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Tanzania (AFP) Soud Said Soud, alisema hata kitendo cha kuunda tume ya uchunguzi hakikupaswa kuwepo kwa sababu ilidhirika mapema kwamba meli hiyo ilijaza abiria na mizigo kuliko uwezo wake.
Alisema mbali na kuchelewesha ripoti, pia chama chake kinapinga kitendo serikali kutochukua hatua dhidi ya wenye dhamana na chombo kilichopata ajali.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), Awadhi Ali Said, alisema kitendo cha serikali kutotangaza ripoti hiyo kina wanyima wananchi haki ya kujua matokeo ya uchunguzi wa ajali hiyo.
“Haki inayokawizwa ni sawa na haki iliyokataliwa,” alisema Awadhi ambaye pia wakili wa Mahakama Kuu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, alisema ripoti ya uchunguzi bado inafanyiwa kazi kupitia ngazi mbali mbali serikalini kabla ya rais kuweka wazi matokeo ya uchunguzi huo.
Alisema ripoti hiyo siyo jambo la kutolewa adharani haraka kwa sababu kabla ya kufanya hivyo kuna vikao mbali mbali, kama vile Baraza la Mawaziri ambavyo vitajadili na kutoa ushauri kabla ya Rais hajatoa taarifa kwa wananchi.
“Baada ya kupoikea ripoti hiyo, Rais bado anatafakari kwa sababu ripoti hiyo siyo nyepesi, inahitaji kuiitafakari kabla,” alisema.
CHANZO: NIPASHE
.jpg)
No comments:
Post a Comment