Wanamuziki ambao wengi wao walishapiga muziki pamoja na marehemu Andy Swebe wakiwa kwenye msiba wa Rafiki yao, pichani ni mkongwe, Sinza Jijini Dar Leo. Pichani ni mkongwe Juma Ubao
Maestro King Kiki ambae alifanya ziara ya kimuziki na Marehemu hizi karibuni Nchini Marekani akiongea jambo kwenye msiba huo, Sinza Jijini Dar leo.
Kulia ni Mwanamuziki Mafumo Bilal akirekebisha mitambo alipokua na wanamuziki wenzake kwenye msiba wa rafiki yao na mwanamuziki mwenzao, Andy Swebe, Sinza Jijini Dar leo.
Wambolezaji waliojumuika pamoja kwenye msiba wa mwanamuziki Andy Swebe uliotokea December 28, 2011 saa 10 alfajiri kwa saa za Tanzania katika Hosipitali ya Marie Stopes iliyopo Sinza, marehemu atazikwa kesho Ijumaa December 30, 2011 Jijini Dar.
Waombolezaji wakiwa kwenye msiba wa Andy Swebe, Sinza Jijini Dar.
Kati ni mwanamuziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la Jaffarai akiwa kwemye msiba wa Andy Swebe, Sinza Jijini Dar leo.
Mwanamuziki John Kitime (shati jeupe kati) akiwa kwenye msiba wa rafiki yake marehemu Andy Swebe, Sinza Jijini Dar Leo.
Wanamuziki mbali mbali waliojumuika pamoja kukesha kwa kupiga muziki kumkumbuka rafiki yao Andy Swebe, Sinza Jijini Dar leo.
(picha kwa hisani ya Richard Maabadi)
No comments:
Post a Comment