ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 21, 2012

Ibada Kiswahili Columbus


Mpendwa Dada/Kaka

Tunapenda kutanguliza salamu za mwaka mpya wa 2012. Tunamshukuru Mwenyenzi Mungu kwa ulinzi wake na baraka alizotujalia mwaka uliopita wa 2011. Mwaka uliopita ulikuwa ni wa mafanikio kwa Ibada ya Kiswahili ambayo ilifikisha miaka miwili. Mafanikio haya yametokana na Sala zako,Mawazo, Juhudi na ushiriki wako binafsi pamoja na waumini wote katika ibada za mwaka jana. 

Lengo letu waumini wa Ibada ya Kiswahili ni kumwabudu na kumtukuza Mungu wetu kwa lugha yetu ya asili ambayo wengi wetu tumekuwa nayo na kuwa mfano kwa jamii zetu zote tukiwapo ugenini. Zaidi ya hilo lengo ilikuwa ni kuimarisha umoja wetu katika kuendelea kumtumikia Bwana wetu Yesu Kristo. Ni mategemeo ya Ibada ya Kiswahili kwamba malenngo haya pamoja na mengine yalifanikiwa na tunakushukuru kwa kuwa mmoja wa waliofanikisha malengo haya. Asante sana na uzidi Kubarikiwa mpaka ushangae.

Mpendwa muumini, mwaka huu wa 2012 Ibada ya Kiswahili itatimiza miaka mitatu. Ni malengo mengi yanayotarajiwa kufanikishwa na yote yatawezekana tukiendelea kuongozwa na Roho Mtakatifu. Tutaendelea kuwa na Ibada ya Kiswahili kila jumapili ya kwanza ya mwezi au zaidi. Huduma na ushiriki wako kwenye Ibada hizi ndio unaofanikisha Ibada ya Kiswahili iendelee kusimama imara katika kumtukuza na kumwabudu Mungu. 

Baadhi ya huduma ambazo Ibada ya Kiswahili inakuhitaji ni kuandaa Ibada (meza ya bwana, kuwasha mishumaa, na kukaribisha waumini),kushiriki Ibadani, kusoma masomo, kuimba kwaya,kuchangia ujumbe Facebook na blog's(Vijimambo,Sunday Shomari na Michuzi), kushiriki Ibada Radioni kupitia www.Radiombao.com, n.k. 

Tunakaribisha na kuyapokea maoni/ushauri wako na pale ambapo ungependelea kushiriki katika kutoa huduma. Mwenyenzi Mungu azidi kukubariki na kuibariki Ibada yetu ya Kiswahili kwa mwaka huu 2012.
Mungu Awabariki!!

Kamati ya Ibada ya Kiswahili – Columbus.

No comments: