Na Faustine Ruta, Bukoba
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu ndie aliyekuwa Mgeni rasmi leo kwenye Ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 za klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom iliyoanza kutimua vumbi hii leo Novemba 15, 2016. Mchezo huu wa ufunguzi uliofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera na kushuhudia Timu wenyeji Kagera Sugar wakiumaliza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Timu ya Yanga.
Kipindi cha kwanza kilimalizika bila ya kufungana, Kipindi cha pili dakika ya 69 Yanga walipata bao la kuongoza kutokana na mpira wa adhabu uliomshinda mlinda mlango wa Timu ya Kagera Samir Mbina Charles. Kipindi cha pili dakika za mwishoni Kagera Sugar walisawazisha bao kupitia kwa Christopher Mshanga baada ya beki wa Yanga kukosea na mpira kumtoka na kujikuta akimsindikiza mfungaji huyo kwenye eneo hatari kwenda kushuhudia bao la kusawazisha kwa Kagera huku zikiwa dakika zimeyoyoma.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu akifanya yake kwenye ufunguzi wa Ligi ya U-20 .


Kagera Sugar U-20
Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar U-20
Msimu wa kwanza wa Timu za U20 umezinduliwa hii leo kwenye Uwanja wa Kaitaba na kushuhudiwa na Mashabiki wengi wa soka na mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1.
Shadrack Nsajigwa ndie alikuwa akiongoza Timu ya U-20 Yanga
Shadrack Nsajigwa mchezaji wa Zamani na hapa akiitumikia Timu ya U20 ya Yanga.
Hakuna kwenda...popote...


katikati ya uwanja patashika lilitokea kipindi cha pili
Yusuph Suleiman(kulia) akimwendesha mchezaji wa Kagera Sugar

No comments:
Post a Comment