ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 13, 2012

Kanisa lachachamaa wachungaji kuhusishwa dawa za kulevya

Sakata la madehebu ya dini kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya limeingia sura mpya baada ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Konde kufungua milango kwa Serikali kuchunguza wachungaji wake kama wanajihusisha na biashara hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Askofu wa Kanisa hilo, Israel Peter Mwakyolile alisema  taarifa kuwa Dayosisi yake imewatimua wachungaji wake wawili kwa tuhuma za kujihusisha na biashara hiyo haramu si za kweli.

Askofu Mwakyolile alisema hajui kama katika kanisa lake hakuna mchungaji yeyote anayejihusisha na biashara hiyo na hajawahi kumfukuza mchungaji wake kwa tuhumahizo, hivyo kama kuna tuhuma za aina hiyo,  Serikali inaweza kuchunguza na ikimbaini mchungaji yeyote anafanya biashara hiyo, imchukulie hatua za kisheria kama raia wengine.
“Katika kanisa langu kwenye Dayosisi ya Konde, sijawahi kumfukuza mchungaji yoyote, lakini mimi sio malaika wala sio Mungu, inawezekana wakawapo mimi siwajui, Serikali inao mkono mrefu ikihisi hivyo milango iko wazi inawea kufanya uchunguzi na ikiwabaini washitakiwe kama raia wengine,” alisema .
Hata hivyo, alisema  kanisa lake linakusudia kulishitaki mahakamani gazeti hilo kwa uwa habari hiyo ambayo ilichapishwa Januari 1 mwaka huu kwa sababu  imewaumiza, kuwajeruhi na kulidhalilisha kanisa lake.
Askofu Mwakyolile pia alitangaza kutomtambua Mchungaji  ambaye alinukuliwa na gazeti hilo kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na haki za jamii, kitengo ambacho alisema kanisa hilo halijawahi kuwa nacho.
Alisema kanisa lake halimjui mchungaji huyo na hivyo linakusudia kwenda mahakamani ili akathibitishe ukweli wa taarifa hiyo aliyoitoa gazetini.
CHANZO: NIPASHE

No comments: