ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 12, 2012

MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 48 YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa jukwaani wakati ukipigwa wimbo maalum wa Taifa wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akikagua gwaride maalum wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali wakiwa jukwaani Uwanja wa Amaan katika Sherehe hizo.
Kutoka (kushoto) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri, Mama Zakhia Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, wakiwa katika sherehe hizo.
Kutoka (kulia) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri, Mama Asha Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Jaji Mkuu, Othman Chande na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakiwa katika sherehe hizo.
Vijana wakipita kwa maandamano na mabango mbele ya Jukwaa Kuu.
Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipita mbele ya Jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni rasmi.
Kikosi cha Polisi  wakipita mbele ya Jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni rasmi.
Kikosi cha kutuliza ghasia FFU, kikipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa haraka na kutoa heshima kwa mgeni rasmi.
Kikosi cha Wanajeshi waenda kwa miguu, kikipita mbele ya Jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni rasmi.

Picha Zote na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: